Thursday, 29 March 2012

SUSUMILA AHAMA MOMBASA

SUSUMILA
Msanii mkali kutoka Mombasa Susumila ambaye hivi maajuzi alitowa wimbo wake mpya akiwa amemshirkisha mkali wa genge, hivi sasa amehama Mombasani na kurejea kwao nyumbani Kilifi.

Baada ya kuzungumza naye katika kikao chetu cha udashdash alieleza  kuwa hivi sasa msanii huyu mwenye ari ya mchwa amesimamisha bonge la nyumba kule county kilifi  ambayo inakisiwa kugharimu hela nyingi tu.

Tulipo muhoji zaidi alisema kuwa alifanya hivyo kutaka kuonyesha wasanii wengine hakuna kitu kisichowezekana unapofanya bidii katika mziki kwani mziki wenyewe unalipa na ukawa na maisha mazuri.pia alisema kuwa familia take inamuhitaji na alifanya hivyo kama jukumu lake kama mtu wa kawaida.

"Ama kweli sililamiki kimaisha bidii yangu ndio imenifanya kuporomosha kitu hiki"
Susumila hivi sasa yuko mbioni kutayarisha video za nyibo zake ambazo hapo awali alikuwa hajazitayarisha.Video inayokuja hivi karibunia ni ile ya wimbo Mikwanja aliyoshirikisha kibzzo.

GROOVE AWARDS WAWEKA WAZI WASHINDANI

Mashindano ya groove awards hapa nchini kenya imefika katika awamo ya 7 mwaka huu, huku ikiendelea kukuza talanta za wasanii wa nyimbo za injili.
hivi maaajuzi katika ukumbi wa nairobi muesum wanadalizi wa groove awards walitangaza nafasi 29 ambazo wasanii watakuwa wakiania:
Nafasi hizi kama:
Msanii bora wakiume wa mwaka                   
DADY OWEN
Daddy Owen
Ekodydda
Holy Dave
Jimmy Gait
Juliani
Man Ingwe


Wimbo bora wa mwaka
Exponential Potential- Juliani
Furifuri- DK and Jimmy Gait
Ghetto- Ekodydda
Liseme- Sarah K
My Call- MOG
Ololo – Emmy Kosgei

Kundi bora la mwaka
Adawnage
JULIANI
BMF
Kelele takatifu
MOG
Maximum Melodies
Tetete

Album bora ya mwaka
Ebenezer – Mercylinah
Kibali – Gloria Muliro
Liseme – Serah K
Ololo – Emmy Kosgei
Pulpit kwa street – Juliani
Utamu wa maisha – Daddy Owen

wimbo bora Hip Hop
Exponential potential – Juliani
KAMBUA
Ghetto – Ekodydda
Mara hio hio – Bantu and Holy Dave
Mmh baba – Kriss ehh baba
Ni msoo – Kelele takatifu and Holy Dave
Press on – Izo and Holy Dave
EMMY

Video bora ya mwaka
Exponential potential – Juliani
Holy Ghost fire – BMF
My call – MOG
Safari – Adawnage
Umetenda – Kambua
Walking – Alemba and Exodus

 Collabo bora ya mwaka
Fresh and clean – Kevo Juice and Jimmy man
Furi furi – DK and Jimmy Gait
My call – MOG and Juliani
Ni msoo – Bantu and Holy Dave
                                               Walking – Alemba and Exodus
                                               Welwelo – Mr Seed and Danco
Na nyinginezo nyingi huku nchi kama Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan ya kusini.
Mafans wote ukiwa unataka kumpigia msanii unaye mwezi kura angalia www.grooveawards.co.ke au www.facebook.com/grooveaward
kumbuka upigaji wa kura unafungwa aprili 27, 2012

Tuesday, 27 March 2012

NYOTA WA TPF WANG'AA AFRIKA MASHARIKI

HEMEDY
Baada ya mkali wa rap collo kumshirikisha mwanadada Ameelena ambaye alikuwa kwenye mashindano ya Tusker Project Fame(TPF) kwa wimbo wake Hodi hodi ambao unakuja kwa kasi kutokana na fleva mpya ndani yake.
Sasa wasaani wengine ambao walishiriki TPF pamoja na Ameelena hapa na mzungumzia king of swag ambrella aka Hemedy ambaye pia mwikizaji wa filamu amekuja na wimbo wake mpya 'Mombasa Queen'.
MSECHU
 Naye Peter msechu pia anayetoka bongo ameangusha kitu kipya kinachojulikana kama 'Unaniumiza' huku akiwa ameshirikisha Belle.

Sasa ni wazi kuwa wasaani hawawaliokuzwa kwenye TPF wanaonesha jinsi walivyo elimika kimziki kwani nyimbo hizi zote ambazo wametoa ni zakiwango cha juu.

MR. NICE AZUA RAPSHA NDANI YA BAA

Toka bongo hivi leo tunamwangazia Msanii maarufu wa muziki wa Takeu Lukas Mkenda maarufu kama Mr Nice, ambaye amechipuka tena kwenye game na wimbo wake ‘Tabia Gani’, juzi usiku aliwashangaza mafans wake alipotupiana makonde mazito mazito na jamaa mmoja ajulikanaye kama John.
Kwa mujibu wa udashdash unaofikia meza yetu ya ketauexpress ni kuwa tukio hilo ambalo lilitokea mida ya saa sita usiku katika baa ya Uhuru Peak iliyopo maeneo ya Mango Garden.
 baada ya msani Nice kufika kwenya bar hio alionekana kimzungumza na John ambaye inasemekana ilikuwa ni jambo kumhusu mpenzi wake Mr. Nice.Wawili hawa waliendelea kurushiana maneno huku Mr Nice akimsakama jamaa huyu almarufu kama John ambaye alimkaripia na kumkanya Nice adharani kuwa hawezi mchukuwa dem wake.
Jambo hili lilionekana kumkera sana mwazlishi wa Takeu ambaye alimzaba jamaa huyu makofi jambo lililosukuma wao kuanza kurishaina makonde kwa dakika 3 hivi kabla ya walinzi wa baa hii kuwatenganisha.


Monday, 26 March 2012

SLIM G BADO ATETA

SLIM G
 Kesi inayomkabili msanii Belle 9 kuhusiana na kucopy wimbo wa msanii Slim G kutoka humu nchini,imefikia kileleni.Slim G amechukulia swala hili kwa undani zaidi na hivi sasa anasema Belle 9 yuko mashakani kwani kesi hiyo imeingia kortini.


 Wimbo najma ulitoka mwaka 2010 ambao ulifanya vizuri katika chati za afrika mashariki,hasa hapa ketau express,ulipigwa tena na msanii belle 9 kuanzia beat mpaka maneno ya wimbo huo.jambo ambalo limemfanya slim G kuchukua hatua ya kumstaki Belle 9.


Ketau express inafuatilia jambo hili kwa karibu.na uhondo tutakupa zaidi.



FAIS NGAZIJA BADO YU MBIONI

Msanii anayekuja kwa kasi kutoka mombasani Fais aka Faiswal Ngazija,ametoa kibao kibya.kibao hicho kinachokwenda kwa jina jipange,ameimba kulingana na hali ngumu ya maisha ilioko sasa.

Akizungumza na ketau express alisema kuwa idea nzima hiyo ni kutokana na hali ngumu ilioyoko miongoni mwa vijana katika sehemu za nchi.


"Ukiangalia vijana wengi hawana ajira ya kujikimu maisha,na ndio maana wimbo huu utawapatia motisha ya kujipanga na kazi yeyote ile"

Fais akiwa ametoa ngoma hiyo mpya,amekamilisha pia video ya wimbo ma biscut ambayo alimshirikisha msanii wa  ragga nchini Fidempa.vedio hiyo tayari imeshaingia katika runinga za humu nchini na ilifanywa na producer Thome wa studio za Boomba.Track zote mbili zilitoka katika studio ya Jungle masters chini ya produce Emmy Dee.
Kongole msanii fais kwani si kazi rahisi kufanya vitu vikali kama hivi.

Tuesday, 20 March 2012

"MAZOEA" YAKE TEMBA APRILI



TEMBA
Toka nyumba ya temeke inayokuza vipaji vingi nchini tanzania hapa na mzungumuzia mkali wa temeke kamanda mtu mzima, namzungumzia Mheshimiwa Temba.
Mheshimiwa Temba hivi sasa amesema yuko mbioni kutoa kazi yake mpya mwezi wa aprili ni kuwa hivi sasa mchizi huyu atakua anatoa wimbo "Mazoea".
kwa mjibu wa temba ngoma hiyo itakwenda samba na video yake na hii itakuwa kazi yake ya kwanza mwaka huu. 

Monday, 19 March 2012

KAGOMAZ WAKAMILISHA ALBUM NA FILANGE

KAGOMAZ
 Kikundi kizama kinachoshirikisha wasanii 3 kutoka Malindi sasa wamekamilisha album yao ya kwanaza ya nyimbo 9.

Nazungumzia kuhusu kikundi cha Kagomaz.Wasanii hawa wametoa kibao kipya kinajulika Filange ambacho kinazungumzia kuhusu maswala ya mapenzi.

"Filange ni vile unavyotamani mrembo wako kuwa karibu na wewe kila wakati,yaani ni hisia na hamu ya kutaka kuwa na mpenzi wako".welowelo aka welo alisema.ambaye ni mmoja wa kundi hilo.

Wimbo  filange vile vile umefanyiwa kazi na studio kadhaa kama vile vocals zake kufanywa katika studio za chill inc chini ya produce Pilipili na beat ikatengenezwa na Bizi B katika studio za S-Bar.

Katika album hiyo kwa jina Mwanzo wa kazi kuimarishwa kwake kumetokana na kazi za maproducer wakali East afrika kama vile Totti kutoka Mombasani,Bizi B,Lil-Gheto kutoka Bongo Benso,Kisaka na Benja.

 hata hivyo msanii welo alifafanua kwamba ngoma katika album hiyo ni 9 lakini kuna bonus track ambazi ni instrumental kutoka kwa ngoma za mbati na Filange.

Wasanii wengine katika kundi hilo ni Meddy pack na Fym.




DIAMOND AFIKIRIA KUIMBA TARAAB


diamond
 Habari za hivi punde toka bongo kumhusu msanii anayevuma sana afrika mashariki Nasseb Abdul aka Diamond ni kuwa anafikiria kuhama toka mitindo ya bongo kimziki hadi kwenye taarab.
Jambo hili linawashangaza mafans wake wengi lakini diamond alinukuliwa akisema kuwa"Hivi sasa katika miziki ya kizazi kipya nko juu tu sana na nina amini kuwa hakuna msanii yeyote kwa sasa, anaweza kufika kiwango nilicho nacho.
Msanii huyo aliongeza kuwa bado hajaamua kufanya muziki huo rasmi lakini anafikiria kama unaweza kumletea soko kama ilivyokuwa kwa bongo fleva, ambao umemfanya ajulikane duniani kote.
“Naweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu nina kipaji cha kuimba nyimbo aina zote hivyo endapo nikifikia muafaka naweza kufanya kitu hicho ingawa mashabiki wangu watastuka sana,” alisema.

Friday, 16 March 2012

TABIA GANI? AULIZA MR NICE.

Msanii toka bongo huyu si mwingine bali ni Mr Nice aka Lucas Mkenda hivi majuzi alitangaza kurudi kwake ulingoni.
Ujio wake kwa mara ya pili sasa una dhihirisha kuwa mwanzilishi wa densi ya Takeu ambayo ina maana tanzania kenya na uganda uko tayari kabisa hii ni baada ya Mr nice kutoa wimbo wake mpya 'Tabia Gani' ambao umeanza kufanya vizuri katika stesheni mbali mbali za redio afrika mashariki.

wimbo huu mpya wake Mr nice umetayarishwa na producer Lamar na video kutengenezwa na Touch of Karabani chini director Karabani.

LEO MADTRAXX AVUKA BODA

KEKO NA MADTRAXX
Make You Dance’ ndio kibao kipya ambacho kiko njiani toka kwa rapper mkali toka uganda ajulikanaye kama Keko ambacho amemshirikisha msani mkali Madtraxx ambaye amevuma sana hapa nchini kenya hasa kwa kibao 'Chake get down' na nyinginezo.
hivi leo Madtraxx yuko nchini Uganda katika harakati za kuuzindua video ya wimbo huo ambao ulitayarishwa na producer mkali toka nchini Nigeria Clanrence Peters mwezi wa februari Nairobi.
Producer huyu wa Nigeria amekua humu nchini toka 2011 akifanya kazi na wasani kama: Love-child Wyre,  Camp Mulla, Banky W, L-Tido, na Bon’eye.  Basi tukingojea wimbo huu kuna kollabo nyingine kali yao Kenyan band Ma na J Cole wakishirikiana na Missy Eliot toka amerika.



HIPHOP KALI TOKA BONGO

Mafans wa hiphop kunakitu kipya kwenu toka bongo kwa wakali wa hip hop ambao baada ya ukimya mrefu wamerejea na 'Tupo Kitaa' hii ni ngoma yake CoinMoko akiwa amemshirikisha Jembe aka BouNako kutoka Nako2Nako soldiers.

Wimbo huu umerokodiwa za noizmekah.com records.
Hivi sasa Bounako yuko jikoni kutayarisha mambo makubwa ambayo ana amini yatakuwa makubwa kwenye indusrty ya hip hop afrika mashariki.

"Kama inavoeleweka ma fans wangu m\wanaulizia kichizi mziki so i hit the booth and did ma thang man!Much respect kwa wote wanaonisupport katika movement ya hiphop music" alisema Coinmoko.

Thursday, 15 March 2012

RADIO AVURUMISHA MAKONDE

radio and weasel
Vituko na visanga vya wasanii wakali wa Goodlfe, hawa si wengine bali ni Radio na Weasal vya endelea nchini uganda.
 Siku ya jumatatu jioni walizua rapsha kali ndani ya bar moja ijulikanayo kama Hi-Table. Vurumai ndani ya jumba hilo la kujistarehesha lilizuka pale Radio alipomwona mtangazaji wa televisheni  Lwasani aka Lubenga Isma.
Lwasani
Vyaanzo vya habari vya eleza kuwa Radio alimvamia maskini Lwasami kwa makonde mazito mazito yaloyomwacha  hoi bila hata ya Lwasama kufahamu kilichokuwa kinajiri.
Huku watu waliokuwa karibu walibaki wamedua,vita viliendelea huku wafuasi wa Googlfe na Lwasama wakikabiliana vikali lakini vikamuuliwa na walinzi wa baa hio.
Muda mchache baadaye Lwasama alionekana akiwa na majeraha mabaya puani na mdomoni.Inasemekana chanzo cha vita hivyo ni kuwa Lwasama alikuwa ametoa matamshi ambayo haya kuwapendeza wana Goodlfe kwenye show yake.
Baada ya kichapo hicho Radio alimwambia Lwasani amfahamishe Eddy kenzo kuwa watampa huduma kama yake, ikiwa atapata visa ya kuwa uingereza wakati wa sikukuu ya pasaka(Easter).

Wednesday, 14 March 2012

BEEF KANDO KWA REDSUN NA PREZZO

CMB PREZZO
REDSUN
Wasani waloikuwa na beef ya chini kwwa chini hapa kenya hawa si wengine bali ni King of dancehall ambaye makao yake ni ufarasa Redsun na Msani aliye kuja upya na wimbo wake 4 sho 4 shizzo CMB Prezzo aka Jakson Makini.
Hivi sasa ni kuwa wasanii hawa wawili wameweka tofauti zao kando na kutupa kitu kipya "sema nao" ambacho hivi sasa kinasambazwa mtanii.

PILIPILI BADO YUKO ULINGONI.....


Ni kwa muda sasa msanii mkali toka kenya Pilipili amekuwa chini ya maji kimziki. mafans wake sasa mna kilahali ya kutabasamu kwani sasa msanii huyu amerejea tena kwa kishindo kibwa.
Pilipili ambaye hivi sasa pia ni producer wa mziki anayefanya viziri amekuja tena na single  mpya "One love" yake Sultry akimshirikisha General Pype.
Hii ni kazi ambayo imepitia kwa mikono yake msanii huyu mwenye kipaji cha aina yake Pili pili.

Monday, 12 March 2012

MR BLUE KUWA BABA


Msanii toka bongo huyu si mwingine bali ni Mr Blue aka Byser ameeleza kuwa anajitayarisha kuwa baba.

kwani anategemea kupata mtoto na mpenzi wake wa zamani anyejulikana kama Wahda Mohamed.

Habari zinazofikia meza yetu ya ketauexpress ni kuwa binti Wahda tayari ashaanza kuvaa nguo pana pana.
kwa hivyo muda si mrefu ataitwa Dingi.

BOBI WINE AMWIIGA KOFI ANNAN

Ghetto president aka Bobi Wine wakati huu amewashangaza mafuns wake alipojitolea kufanya mazungumuzo ya amani nchini uganda kati ya makundi mawili tata nchini Uganda.
Hii ni kati ya kiongozi wa mapinduzi Joseph Kony na serikali ya uganda ilikuleta amani nchini uganda, huku kampaini kali inayoendeshwa na wanaharakati wa amerika katika mtandao wanaodai kuwa kiongozi huyu wa kundi haramu la Lords Restance Army linalowahangaisha wakaazi wa kusini mwa uganda anastahili kutiwa mbaroni.




Thursday, 8 March 2012

EDDY KENZO AWEKA WAZI "OGENDA KUNZIA" NA MAMA SUKARI


kenzo
Baada ya wasanii wakali toka goodlife nchini Uganda radio na weasel kumsaidia msanii chipukizi anayekuja kwa kasi Boerman kurekodi wimbo mojawapo ya kenzo ‘Ogenda Kunzia’ Huku boerman akidai kuwa wimbo huu ulikuwa wake naye Kenzo ameuiga toka kwake.

Sasa hivi meza ya ketauexpress imegundua wimbo huu ‘ogennda kunzia’ wenye utata uliotungwa naye Kenzo ulilenga hali halisi ya maisha yake, baada ya kutishiwa maisha yake na mwanamumme anayekisiwa kuwa mpenzi wa aliyekuwa (sugar mom) mom Halima.


Katika wimbo wenyewe Msanii kenzo anayevuma na kibao ‘Bolingo’ analalamikia jinsi anavyokerwa na jumbe anazotumiwa na mwanamume huo.Licha ya kuwa si yeye alimlaghai.Ndani ya wimbo wenyewe kenzo anazidi kueleza jinsi mpenzi wake mama Halima anavyomwonya aachane naye,ijapokuwa ni mama sukari Halima anajipendekeza kwake.
radio and weasel

2010 tetesi kuhusu sakata ya mama sukari ilikuwa inamkabili kenzo wakati alipokuwa anaanza mziki, naye aliliweka siri.Inakisiwa kuwa mama Halima ndiye aliye gharamia nauli za usafiri za kenzo na pia alimpa pesa nyingine za matumizi.
Lakini baada ya kenzo kuuza haki miliki za nyimbo zake kwa promoter Balaamu na kujiunga na kampeini ya kuuza wimbo wake 'Stamina'.Hapo ndipo msanii Kenzo alimwaga mama sukari Halima na kutomtegemea kabisa.

Wednesday, 7 March 2012

ALFAYO NA CARTEL"NYERIFICATION"


Wasanii wakali kutoka katenga production  Alfayo na Cartel wamekuja tena na wimbo wao mpya unaozungumzia matatizo yanayo kumba wapenzi katika ndoa zao.

Hivi sasa mitaani wengi wanawaita wasanii hao wawili “NYERIFICATION” au “djemo thako" kumaanisha (baba ampiga mama) kwa lugha ya kiswahili.

wasanii hao kutoka kundi la katenga wametunga wimbo huu kupinga matatizo ya ndoa na kutumia njia mbadala kusuluhisha matatizo ya ndoa ambayo ni mazungumzo.

Hata hivyo katenga wanawahimiza mafans wasikize wimbo wao. Huku wakizingatia kuishi kwa amani na kuheshimu ndoa zao ilikukuza jamii hasa watoto wao.

KIZAA ZAA CHA MAGWIJI

BEBE COOL
BOBI WINE
Wasanii wanaojulikana kwa beef kali nchini Uganda hivi sasa wajiandaa kufanya tamasha pamoja mwezi  Aprili linaloandaliwa na wadhamini (mapromoter) Emman Serugo na Musa Kavumamkali kutoka Uganda.
Kulingana na wadadisi,Bobi Wine aka Ghetto Gladiator aka Omubanda wa Kabaka(Kings Gangster) na Bebe Cool wanasemekana kuwa ni marafiki lakini kutumia beef yao kuwapumbaza mashabiki wao.

Tamasha hiyo itaandaliwa katika kumbi za  Hoteli Africana iliyoko Resort beach. Hii itakuwa tamasha ya pili ikizingatiwa ya kwanza ilikuwa kati ya Bobi Wine na mwanawe Mayanja aka Dr. Jose Chameleone.

Akiongelea jambo la tamasha hiyo Bobi Wine alisema, iwapoatashirki kwenye mchuano huo atachukua 85% ya pesa zitakakusanywa kwenye tamasha hilo.Bado haijadhibitishwa iwapo Bebe Cool atakubali 25% itakayosalia.





DADDY OWEN AJIONDOA GROOVE AWARDS



Msanii anaye vuma wa gospel Daddy Owen amewashangaza mafans wake baada ya kujiondoa katika tuzo za Groove award.
Daddy Owen alisema kuwa tayari yeye ashashiriki katika tuzo za groove na akapata tuzo kadhaa na anachukuwa fursa hii kuwapa wasaani wanaochipuza nafasi ya kushiriki katika tuzo za Groove ambazo hutolewa kwa wasanii wa miziki ya injili.
Katika tuzo za Groove award za 2011 Daddy Owen aliibuka msanii bora alipotoka na tuzo nne zikiwemo msanii bora wa mwaka, wimbo bora wa mwaka, video bora ya mwaka na collabo ya mwaka, na wimbo wake "Saluti."
Huku Daddy Owen akimpa Juliani tuzo yake ya msanii bora, jambo ambalo ni nadra sana kwa wasanii wa kenya.

Tuesday, 6 March 2012

BARNABA ATAYARISHA ALBAMU MPYA

Barnaba
Toka nyumba ya vipaji bongo THT msanii Barnaba ambaye hivi sasa anatayarisha video kali ya wimbo wake Gube gube."Video hii itakuwa ni ya kisasa na itafikia viwango vya kimataifa"Barnaba aliendelea kusema kuwa yuko mbioni kufanya maandalizi ya albamu yake mpya.
Alisisitiza kuwa habari kamili kuhusu track zitakazo kuwa kwenye albamu hio zitajulikana aprili na nyinbo tano ndizo zitatengeza album hio ambao Barnaba anahisi itakuwa na mdundo wa aina yake.

Saturday, 3 March 2012

BELOW MSIMU WA ELIMU

Tongwe Records inafurahia kukuletea wimbo mpya BELOW uliofanywa na  BARAKA akimshirikisha  R.O.M.A na CHEGE chini ya producer J-Ryder.

Hii ni baada ya Matoleo ya Mtihani wa Kidato cha nne ambayo wanafunzi wengi hawakufuzu. Waliamua kuufanya wimbo huu ilikuuliza ni nani mwenye makosa, Je ni Mwanafunzi? mwalimu? Mzazi? Serekali ama Msimu wa Elimu wenyewe.

Chege

Wasanii hawa wanatumahi kuwa wimbo huu utamgusa yeyote mwenye makosa na kurekebisha ili kuboresha elimu Tanzania.




UJIO WA BLU3

BLU3
Kundi la wasanii wa kike kutoka Uganda sasa linaaminika kurudipamoja kimziki baada ya migogoro iliyofanya kusambaratika kwa kundi hilo. Mabinti hawa watatu pamoja na Mkurugenzi wao Steve Jean wa Fenon Records wamo kwenye maongezi yatakayo unganisha kundi hili tena.

Cindy aliyepigwa kalamu 2008, Lillian na Jackie anavuma kwa kibao chake gold digger, watarekodi na kutumbuiza mashabiki wao kwa pamoja sasa.

Cindy alipoondoka, Mya Baganda ndiye alishikilia nafasi yake lakini baadaye akajifungua mtoto. Lillian kwa upande mwingine anasusiwa kuwa mjamzito na mtoto wa pili wa Moze Radio. Msanii huyu amekuwa akijishughulisha na band yake ya Sundowners, ni Mtangazaji kwenye Radio City, mzazi na sasa kundi la Blu3 kufufuka itakuwaje?