MSANII PROFILE

MEJJA
Mejja Meme Hadhija ni mmoja wa wasanii bora nchini.
Alianza kuimba akiwa bado katika shule ya msingi. Yeye na ndugu yake, Wambugu, walijiunga na kundi la waimbaji la Ghetto Clan.
Baadaye akaungana na producer wake Clemo na kuanzia kazi ya usanii na kutoa kibao chake cha kwanza, Jana kuliendaje ilivuma kote nchini na akaweza kuibuka kuwa mshindi katika Chaguo la Teeniz.
Kisha akajiunga na Calif Records, ambayo inajulikana kuwa na wasanii kama Jua Cali, na producer wao Clemo.
Hivi majuzi ametoa wimbo wa Landlord ambao hadi sasa umeendelea kuvuma kote nchini.




REDSAN

 Redsan (jina lake kamili ni Swabri Mohammed) ni msanii wa ragga na reggae kutoka Kenya. Alizaliwa mwaka 1981.
Alianza kazi yake ya usanii baada ya kushinda shindano la Star Search katika uwanja wa Carnivore, Nairobi mwaka 1998.
Alikuwa mmoja wa wanamuziki mashuhuri wa Ogopa DJ's.
Alijiunga na Lucas Bikedo kutoka Sing Sounds, kabla ya kuanzisha Ogopa DJ's. Baadaye alianzisha East African Bashment Crew wakisaidiana an Chameleon na Bebe Cool, wote kutoka Uganda.
Album yake ya kwanza, Seasons of the San, ilitolewa mnamo mwaka wa 2002 na Ogopa DJ's. Seasons of the San ilikuwa na nyimbo tisa. Kati ya hizo tisa zilizovuma sana ni "Julie" na "Wanipa Raha".
Baadaye alihamia Southwest Records alipotoa album yake ya pili, Red, mnamo mwaka wa 2004. Ilikuwa na nyimbo kama vile "Chicken" na "Apakatwe".
Album yake ya tatu, Pioneer, iliyotolewa mnamo mwaka wa 2006, ikiwa na nyimbo kama "Kenyan" na "Touch".
Baada ya kutoa nyimbo kadhaa, Redsan aliamua kuunda kundi lake la Dutty Sounds. Kundi lenyewe linahusha wanamuziki wa dancehall, hiphop na R&B.
Redsan amezuru baadhi ya mataifa kama Marekani na Ulaya.
Amejishindia taji la Chaguo La Teeniez na Kisima kama msanii bora Kenya.






AMANI
Amani, ambaye kwa jina lake hasa ni Cecilia Wairimu, alisaidiwa na Redsan kutoa wimbo wake wa kwanza, move on,  mwaka 1999.
Katika mwaka 2002 alifanya collabo na Nameless na kutoa wimbo wa ninanoki ambao ulimfanya kutambulika kama msanii bora Afrika Mashariki. Huo wimbo ninanoki ulipendwa sana  na mashbiki wake kote Afrika mashariki na magharibi.
Alitoa wimbo wa papi mwaka 2003 ambao ulichezwa sana Uganda, Tanzania na Malawi.
Kisha akafanya collabo na Bigpin na Patonee na kutoa wimbo talk to you na mwaka 2006 akatoa wimbo uliofahamika kama tamani.
Alishinda tuzo la kuwa msanii bora wa kike katika  Mama MTV music awards



 JUA KALI


Wimbo wake wa kwanza kabisa kurekodiwa ulikuwa Ruka, uliotolewa mwaka 2001 na ukafuatiwa na Nipe Asali mwaka wa 2002.Katika mwaka wa 2004 yeye na PiliPili walitoa wimbo ‘Kamata Dame’.Kama wasanii wengine wa Kenya, ilimchukua miaka kadhaa kabla ya kuitoa albamu yake ya kwanza kamilifu.Albamu yake ‘Juacali Sekta’ ilitokea mwaka wa 2006, ikizijumlisha nyimbo zake za hapo awali.
Wimbo ‘Kwaheri’ akijumlisha Sanaipei ulitia fora sana nchini Kenya mwaka wa 2007.Kwenye mkesho wa mwaka mpya 2008/2009 alitoa albamu mpya, ‘Ngeli ya Genge’.Jua Kali amezuru Amerika na pia mataifa mengine mnamo Agosti 2007, alikuwa kati ya watu 100 mashuhuri nchini Kenya, hii ni kulingana na gazeti la The Standard
Jina lake la uimbaji Jua kali lilitwaliwa kutoka jina California, eneo lililoko Kenya kama katika jina Calif Records. Pia ni  jina ambalo hutumika kumaanisha viwanda vya chini katika uchumi wa Kenya
Kando na kuwa na talanta ya uimbaji.Amefanikiwa katika mambo ya biashara, haya yote yamechangiwa na kupendwa kwake na vijana pamoja na wale walio na umri ambao si mdogo sana.Alikuwa msanii wa kwanza Mkenya kupata tuzo la biashara, mwaka wa 2007, la shilingi milioni moja za Kenya na kampuni kuu ya simu za rununu ya Motorola kwa ajiri ya simu zake za muundo wa Motorola.

 NONINI


Hubert Nakita ambaye anafahamika kama Nonini ni miongoni mwa wanamuziki maarufu walioko humu nchini.Nonini alizaliwa oktoba 2 1982. Ni msanii anayeimba kwa mtindo wa Genge na hiphop na amekuwa akirekodi nyimbo zake nyingi Calif records
Nonini amekuja julikana katika sanaa ya mziki single yake "Nonini you Nani?"
2002 baada ya kutoa wimbo "manzi wa nairobi" alianza kufahamika kikamilifu kimziki na kisha baadaye tena akaangusha kibao kingine "Wee kamu".
2004 Nonini alitoa ablum yake ya kwanza ulio fahamika kama Hanyaring Game ambao ilikuwa imejumuisha hit song yake "Keroro"

2007 Nonini alitoa album yake ya pili iliyofahamika "Mwisho Ya Mawazo" ambayo ilikuwa na nyimbo zake kali. Baaada ya Nonini kutoa kollabo ya "Nani Mwenza" na mkali wa bongo Juma Nature na wimbo huu kuwa hit afrika mashariki.
Amefanya collabo na Nameless na kutoa wimbo wa ''Furahi Day'' ambayo ilipokewa na mashabiki wake kwa wingi.
Albamu yake ya pili ni "Mwisho Wa Mawazo" ambayo aliitoa mwaka 2007  mwezi Agosti ambayo aliwashirikisha wasanii kadhaa kama vile Nyota Ndogo, Mercy Myra, Professor Jay na Q-Chief.

Alifanywa kuwa ambasada wa International Lifestyle katika chuo kikuu cha Limkokwing huko Malaysia.
Amejitolea kuwasaidia na kuwaendeleza wasanii wanaotamani kujiendeleza kimuziki.
2008 akaunda kundi la waimbaji la P-Unit (Pro-Habo unit) ambayo ina wasanii kama vile Bonnie Frash Gabu. P-Unit wametoa nyimbo kama Si Lazima, Kushoto-Kulia, Kare na Gentleman ambao ulitolewa hivi majuzi.
Baadhi ya Albamu za Nonini ni:
Hanyaring Game(2004)
Mwisho wa Mawazo(2007)

Nonii pia amekuwa akipiga vita uhasamaa unaofanyiwa mazeruzeru afrika mashariki na kusaidia katika mradi huu akatunga wimbo wake "Colour kwa face" inayotetea haki zao.



NAMELESS

namelessNameless-David Mathege ndio majina yake kamili alizaliwa mwaka wa 1976.
Msanii Nameless amekuja kujulikana kwenye sanaa ya mziki mwaka wa 1999 kufuatia tamasha la kutafuta talanta katika stesheni ya radio ya Capital fm ambayo msanii nameless alikuwa mshindi na wimbo wake  “Megarider”.
2001 Nameless alitia kandarasi na Ogopa dj's label na huko ndiko alikutana na wasanii kama vile marehemu E-sir na wakatoa kollabo  “Boomba Train”.
2002 alitoa kolabo nyingine iliyokuwa hit akiwa amemshirikisha mwanadada Amani na mwaka wa 2004 Nameless alitoa albuma yake ya kwanza iliyofahamika kama ‘On Fire’ hili lilimfanya awe miongoni mwa watu 100 mashuhuri nchini Kenya mwaka 2007.

TUZO
2009 Nameless alishinda tuzo mbili za MTV Africa Awards
Namless alikuwa msanii bora wa kiume na wimbo wake “Sunshine”chaguliwa kama wimbo unaosikizwa na wingi.
Hizi ndizo nyimbo ambazo msanii nameless ametayarisha katika safari yake kama msanii
Sinzia,
Sunshine(na habida),
Karibia,
Salary,
Greedy(na kidum),
Friday(na nonini),
Juju(na mr leni),
Prisioner(na blue30
Coming Home
Huku coming home ukiwa ndio wimbo wake alioutoa hivi karibuni.


LADY JAYDEE

Lady Jaydee ni msanii wa R&B kutoka Afrika Mashariki na jina lake halisi ni Judith Daines Wambure Mbibo. Anajulikana pia kama Binti Machozi.
Ana uewezo wa kuimba kwa lugha tofauti kama vile Swahili, Zulu, Lingala, Kintarwanda, French na Kiingereza.
Moja ya nyimbo zake maarufu zaidi, Distance, aonekana kutumia lugha hizo zote kutunga huo wimbo.
Ana Albamu kadhaa kama vile Binti, Moto, Shukrani, Ya 5 na zinginezo.
Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni Machozi, Mawazo, Nishike Mkono, Tatiza, Pumziko, Ukoo Juu, Waweza kwenda ma umuhimu wako, Siku Hazigandi, Siri Yangu, na Usiuseme moyo





 PROFESSOR JAY
 Joseph Haule, kazaliwa December 29, 1975 anayefahamika kama Professor Jay, ni mwanamziki kutoka Bongo anayeimba nyimbo zake kwa mitindo wa hip hop.
 
HISTORIA YA MZIKI
Hapo awali Msanii proffesor Jay alikuwa katiak kundi la Hard blasters ambalo lilianza mziki mwaka wa 1994 na wakavuma na kujulikana na vibao vyao kama Chemsha Bongo huku Professor Jay wakati huo alijulikana kama Nigga J.Na baada ya mwaka mmoja kundi hili lilipata tuzo la kundi bora la hip hop Tanzania.

Mwaka 2001 Proffesor Jay aliamua kujisimamia kimziki na kuanzisha taaluma yake ya mziki solo na hapo akalitupa jina la Nigga Jay kwenye kaburi la sahau na kuja na jina analotumia hivi sasa kama Professor Jay aka waziri wa mitulinga .

Wakati huu alipokuwa akifanya mziki kama 'solo artist' Jay aliangusha vibao kama Nikusaidiaje na Zali La mentali ambazo zilikuwa hit kali aftrika mashariki.
Jay ni msanii ambaye yupo juu tu sana nchini Tanzania  katika mitindo wa kufoka foka ama ukipenda hip hop licha ya kuchipuza kwa wasani wengine wa hip hop nchini tanzania hakuna msanii hivi sasa ambaye anaweza kufikia tajriba ya Professa Jay.

kufikia sasa Msanii Jay ametoa nyimbo zaidi ya ishirini zinazo julikana sana na mafans wake nyimbo hizi ni kama Nikusaidiaje (akishirikiana Ferooz), Nimeamini (ft lady jay dee), Inatosha (ft sugu), Vuta raha (ft Ferooz), Border kwa border (ft Nazizz), Heka heka za star, Interlude, J.O.S.E.P.H., Nisamehe (ft Banana), Wapi nimakosea, Una, Hakuna Noma, Jina Langu, Bongo Dar Es Salaam, Piga Makofi, Msinitenge, Sio Mzee, Zali la Mentali, Nidivyo Sivyo, Mtazamo (ftAfande Sele and Solo Thang).
Solo albums za Jay
  • Machozi Jasho na Damu 2001
  • Mapinduzi Halisi 2003
  • J.O.S.E.P.H 2006
  • Aluta Continua 2007

Tuzo

  • 2004 Tanzania music Awards (Kilimanjaro Music Awards)- Best Hip Hop Album ("Mapinduzi Halisi")
  • 2006  Tanzania music Awards- Best Song (Nikusaidiaje)
  • 2006 Tanzania music Awards - Best Tanzanian Song (Nikusaidiaje)
  • 2006 Tanzania music Awards - Best Ugandan Song (Sivyo Ndiviyo with Chameleone
  • 2007 Pear of Africa awards (PAM Awards) - Best Male Artist (Tanzania)
  • 2009  Tanzania music Awards- Best Songwriter
Hivi sasa Professa Jay amerudi juu kwenye chati na wimbo wake mpya unaofahamika kama Kamili Gado ambao unafanya vizuri sana afrika mashariki wimbo huu amemshirikisha msanii Marco chali.

KAGOMAZ
11/4/2012
Kundi nzima la Kagomaz ni kundi la wasanii watatu wennye kipaji cha mziki kutoka nairobi. Kundi hili la kagomaz lilibuniwa mwaka wa 2006 huku likiwa na wasani kama.
MEEDY
FYAM
WELLO
kundi hili la kagomaz lina uwezo wa kipekee wa kutunga nyimbo kwa lugha tofauti tofauti huku wa kiipa mziki fleva tofauti kabisa.
kindi lina uwezo wa kuimba kiswahili,kingereza,kitaliano,kifaransa huku wakizingatia mititindo ya uimbaji kama vile Bongo flava,Genge,Salsa,R&B,Zouk,Ragga,Dance Hall.
 Huku kundi hili likiwa chini ya uongozi wa CHILLI INC na KAGOMAZ.

ABLUMU NA NYIMBO ZAO

  • Jewe ntarira
  • Nitarudi
  • Amore mio
  • Shemeji
  • Sasa mi ft Reina
  • Mbatii
  • uswazi ft kagomaz-True love
  • Filange
 Hivi ngoma inayovuma ya Kagomaz ni Filange ambayo imezinduliwa hivi karibuni sasa ipo live katika steheni nyingi za radio na tegea live ndani ya ketauexpress kbc radioa taifa na Mtetezi upate kibao hiki .
Kagomaz pia wameanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kukuza talanta za wasanii chipukuzi huku wakiwa namiradi mingine ya mauzo ya mavazi yenye logo kali ya kagomaz
Kagomazi wamewaahidi mafans kuwa wawe tayari kwani hivi punde wanaangusha album ya nyimbo 11.

 CANNIBAL 
10/4/2012
CANNIBAL
Hivi leo ndani ya ketauexpress tunamwangazia Msanii Cannibal mkali toka mombasa kama avyojiita mwenye Mfalme wa Mombasa.
leo amekuwa live katika meza ya ketauexpress na alikuwa na haya ya kusema kutokana na career yake ya mziki.
HISTORIA YA MZIKI
Anakumbuka vizuri kujulikana kwenye industry mwaka wa 2005 akishirikiana na ndugu yake  wa karibu kimziki Sharama walipovurumisha vibao kama Kichwa kibovu na Bouncing.

Kwa muda mrefu msanii Cannibal amekuwa ametulia kimziki hapa alikuwa amepata mialiko kadha ugaibuni kupiga show na muda mwingi alikuwa katika makao yake rasmi mombasni akitayarisha nyimbo zake .
hivi sasa Cannibal amezuka tena kwenye chat ya mziki afrika mashariki ujio wake unaotambulikana sana ni wake msanii escobar toka mombasani.

Mwaka wa 2011 Cannibal tena akazuka na collabo ambao ilikuwa heat katika stesheni nyingi za radio afrika mashariki.wimbo huu ulijulikana kama My REASON ambayo alikuwa ameshrikiana na mwanadada Abida msanii toka Mombasa.

Mwanzo wa 2012 Cannibal aliamua kuungana naye mkali  king of bling bling aka Prezzo na kuanzisha kundi
nzima la mziki linalojulikana kama MMG ambacho hivi sasa wametoa ngoma kali chini ya muungano huu unaojulikana kama 'Ma city Ma Town'.

Hivi leo msanii Cannibal amefunga wazi na kuwahidi mafans wake wataragie album kali toka kwake ambao atakuwa na ngoma 20 album hii itajulikana kama PRODIGAL SON.

Kazi ya hivi punde ya Cannibal ni kuwa hivi sasa anashuhulikia wasani wa chipukizi kwa kuwapa mawaidha kimziki kama vile kuwafunza kuandika mziki ya mtindo wa hiphop na hata kufanya nao kolabo.



MTETEZI

No comments:

Post a Comment