Monday, 19 March 2012

KAGOMAZ WAKAMILISHA ALBUM NA FILANGE

KAGOMAZ
 Kikundi kizama kinachoshirikisha wasanii 3 kutoka Malindi sasa wamekamilisha album yao ya kwanaza ya nyimbo 9.

Nazungumzia kuhusu kikundi cha Kagomaz.Wasanii hawa wametoa kibao kipya kinajulika Filange ambacho kinazungumzia kuhusu maswala ya mapenzi.

"Filange ni vile unavyotamani mrembo wako kuwa karibu na wewe kila wakati,yaani ni hisia na hamu ya kutaka kuwa na mpenzi wako".welowelo aka welo alisema.ambaye ni mmoja wa kundi hilo.

Wimbo  filange vile vile umefanyiwa kazi na studio kadhaa kama vile vocals zake kufanywa katika studio za chill inc chini ya produce Pilipili na beat ikatengenezwa na Bizi B katika studio za S-Bar.

Katika album hiyo kwa jina Mwanzo wa kazi kuimarishwa kwake kumetokana na kazi za maproducer wakali East afrika kama vile Totti kutoka Mombasani,Bizi B,Lil-Gheto kutoka Bongo Benso,Kisaka na Benja.

 hata hivyo msanii welo alifafanua kwamba ngoma katika album hiyo ni 9 lakini kuna bonus track ambazi ni instrumental kutoka kwa ngoma za mbati na Filange.

Wasanii wengine katika kundi hilo ni Meddy pack na Fym.




No comments:

Post a Comment