Thursday, 15 March 2012

RADIO AVURUMISHA MAKONDE

radio and weasel
Vituko na visanga vya wasanii wakali wa Goodlfe, hawa si wengine bali ni Radio na Weasal vya endelea nchini uganda.
 Siku ya jumatatu jioni walizua rapsha kali ndani ya bar moja ijulikanayo kama Hi-Table. Vurumai ndani ya jumba hilo la kujistarehesha lilizuka pale Radio alipomwona mtangazaji wa televisheni  Lwasani aka Lubenga Isma.
Lwasani
Vyaanzo vya habari vya eleza kuwa Radio alimvamia maskini Lwasami kwa makonde mazito mazito yaloyomwacha  hoi bila hata ya Lwasama kufahamu kilichokuwa kinajiri.
Huku watu waliokuwa karibu walibaki wamedua,vita viliendelea huku wafuasi wa Googlfe na Lwasama wakikabiliana vikali lakini vikamuuliwa na walinzi wa baa hio.
Muda mchache baadaye Lwasama alionekana akiwa na majeraha mabaya puani na mdomoni.Inasemekana chanzo cha vita hivyo ni kuwa Lwasama alikuwa ametoa matamshi ambayo haya kuwapendeza wana Goodlfe kwenye show yake.
Baada ya kichapo hicho Radio alimwambia Lwasani amfahamishe Eddy kenzo kuwa watampa huduma kama yake, ikiwa atapata visa ya kuwa uingereza wakati wa sikukuu ya pasaka(Easter).

No comments:

Post a Comment