Msanii anaye vuma wa gospel Daddy Owen amewashangaza mafans wake baada ya kujiondoa katika tuzo za Groove award.
Daddy Owen alisema kuwa tayari yeye ashashiriki katika tuzo za groove na akapata tuzo kadhaa na anachukuwa fursa hii kuwapa wasaani wanaochipuza nafasi ya kushiriki katika tuzo za Groove ambazo hutolewa kwa wasanii wa miziki ya injili.
Katika tuzo za Groove award za 2011 Daddy Owen aliibuka msanii bora alipotoka na tuzo nne zikiwemo msanii bora wa mwaka, wimbo bora wa mwaka, video bora ya mwaka na collabo ya mwaka, na wimbo wake "Saluti."
Huku Daddy Owen akimpa Juliani tuzo yake ya msanii bora, jambo ambalo ni nadra sana kwa wasanii wa kenya.
No comments:
Post a Comment