![]() |
BLU3 |
Kundi la wasanii wa kike kutoka Uganda sasa linaaminika kurudipamoja kimziki baada ya migogoro iliyofanya kusambaratika kwa kundi hilo. Mabinti hawa watatu pamoja na Mkurugenzi wao Steve Jean wa Fenon Records wamo kwenye maongezi yatakayo unganisha kundi hili tena.
Cindy aliyepigwa kalamu 2008, Lillian na Jackie anavuma kwa kibao chake gold digger, watarekodi na kutumbuiza mashabiki wao kwa pamoja sasa.
Cindy alipoondoka, Mya Baganda ndiye alishikilia nafasi yake lakini baadaye akajifungua mtoto. Lillian kwa upande mwingine anasusiwa kuwa mjamzito na mtoto wa pili wa Moze Radio. Msanii huyu amekuwa akijishughulisha na band yake ya Sundowners, ni Mtangazaji kwenye Radio City, mzazi na sasa kundi la Blu3 kufufuka itakuwaje?
No comments:
Post a Comment