Tuesday, 27 March 2012

MR. NICE AZUA RAPSHA NDANI YA BAA

Toka bongo hivi leo tunamwangazia Msanii maarufu wa muziki wa Takeu Lukas Mkenda maarufu kama Mr Nice, ambaye amechipuka tena kwenye game na wimbo wake ‘Tabia Gani’, juzi usiku aliwashangaza mafans wake alipotupiana makonde mazito mazito na jamaa mmoja ajulikanaye kama John.
Kwa mujibu wa udashdash unaofikia meza yetu ya ketauexpress ni kuwa tukio hilo ambalo lilitokea mida ya saa sita usiku katika baa ya Uhuru Peak iliyopo maeneo ya Mango Garden.
 baada ya msani Nice kufika kwenya bar hio alionekana kimzungumza na John ambaye inasemekana ilikuwa ni jambo kumhusu mpenzi wake Mr. Nice.Wawili hawa waliendelea kurushiana maneno huku Mr Nice akimsakama jamaa huyu almarufu kama John ambaye alimkaripia na kumkanya Nice adharani kuwa hawezi mchukuwa dem wake.
Jambo hili lilionekana kumkera sana mwazlishi wa Takeu ambaye alimzaba jamaa huyu makofi jambo lililosukuma wao kuanza kurishaina makonde kwa dakika 3 hivi kabla ya walinzi wa baa hii kuwatenganisha.


No comments:

Post a Comment