Tuesday, 10 July 2012

BIBILIA ALIYOACHIWA NA MAMAKE MSANII AY

AY
Msanii kutoka bongo anayejulikana kama AY anatuarifu kuwa yeye huzunguka na bibilia yake alioachiwa na marehemu mama yake kila mahali aendako.
Msanii huyo wa kizazi kipya alisema mamake alimwachia biblia ambayo tangu akaabidhiwe mkononi hajawahi kuiacha kila anaposafiri kwenda mikoani ama nchi za nje kupiga show ama shughuli za kibinafsi basi biblia hiyo lazima iwemo kwenye begi lake. anasema hawezi lala kabla yeye kusoma vifungu kadhaa kutoka kwa bibilia hiyo hata ikiwa amepiga mitungi yake
Msanii huyo humfanyia ibada kanisani mamake kila wakati wa ukumbusho. anadai kuwa wakati mmoja siku hiyo muhimu ilimpata Moscow na ikawabidi watayarishi wake wa fanye juu chini ili kupata kanisa na AY afanye ibada hiyo.
Msanii huyo ameonyesha heshima na upendo mkubwa aliyokuwa nao kwa mamake mzazi  

Monday, 9 July 2012

MSANII MB DOG ARUDI NA MUZIKI MPYA

MB DOG
Baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye ramani ya muziki hatimaye msanii wa kizazi kipya Mb Dog amerudi kwa kishindo na kibao kipya kinachojulikana kama 'The Only One'.
Alitayarisha wimbo huo kwa studio yake mwenyewe aliyofungua hivi majuzi, Makopa inc.
Msanii huyo aliyetamba zamani na kibao 'Latifa' amesema kwa muda mrefu alikuwa akifanya mambo yake nchini Ujerumani na sasa ameamua kurudi rasmi kwenye muziki
Mb Dog anadai kuwa hana wasiwasi kuwa ataigusa tena  nyoyo za mafaans wake wa Tanzania kwa kuwa haoni kipingamizi chochote na muziki hauja badilika sana.
Msanii huyo alidai kuwa kibao chake kipya kinaweza kuwa zaidi ya kile cha Latifa.

Friday, 6 July 2012

MSANII JAQUAR AOKOA

JAQUAR

Msanii wa kizazi kipya Jaquar aamua kumfadhili msichana mmoja katika masomo yake. 
Wawili hawa walikutana katika mitaaa ya mabanda ya mukuru  wakati msanii huyu alikwenda kwa matayarisho ya video yake mpya ya wimbo Matapeli
Msichana kwa jina Jackline Wanjiku alimweleza Jaquar kuwa alipata nafasi katika chuo cha Walimu Cha Sunrise Athi River. Lakini hakuweza  kujiunga na wenzake kutokana na ukosefu wa fedha. Hivyo  basi baada ya msanii huyu kumsikiza jackline kwa maakini aliamua kumsaidia na kumlipia karo kwa masomo yake

Thursday, 5 July 2012

PREZZO HUENDA AKAAGA BBA


PREZZO
Msanii maarufu nchini  Prezzo au King of bling huenda akayaaga mashindano ya Big Brother Africa wiki hii kama hatopata kura za kutosha kutoka kwa mashabiki wak.
Hii si habari nzuri kwa Prezzo ambaye hivi karibuni ametokea kuwa adui wa nchini zingine za Afrika,kama vile Nigeria,Ghana na Afrika kusini.
Wakati mmoja msanii huyo alileta vurumai  akimtusi Goldie ambaye walikuwa karibu sana na kufanya watazamaji wa Nigeria kumchuku kupindukia baada ya, Prezzo kumtaja Goldie katika nominations ili atolewe kwenye shindano hilo kitu ambacho kimewafanya aonekane msaliti na watu wa Afrika Magharibi kujiunga na Afrika Kusini kuchukia na kuponda chochote anachofanya Prezzo.
Mbali na Prezzo kuwa katika kikaango hicho cha kufurushwa wengine  Lady May, Kyle, Goldie, Junia na Keagan wa Afrika Kusini.
Sisi hapa tunaomba nchi za Tanzania na Uganda kumuokoa Prezzo ili kunyakua ubingwa wa BBA.

NISSI THE BAND KENYA IMEKUJA RASMI

NISSI THE BAND
Kundi la Nissi The Band Kenya ni kundi linalokuja kwa kasi ki mziki wa injili katika miondoko ya kizazi kipya.
Kundi hili linaloongozwa na Jimmy Gachu aka J Moo limerekodi ngoma mpya inayojulikana "Moyo Wangu"katika studio za Talent Entertaiment chini ya produza Elly Zee hapa jijini Nairobi.
Katika hali ya kujizatiti kimziki,kundi hili limetoa album inayoitwa "Mabawa"iliyo na ngoma sita zikiwemo Baba Yangu,Mabawa,Mpenzi,nyingine zikiwa kwa lugha ya Kikuyu kama vile Ihua(Rose) na Makaya(Kilio).
Hata hivyo  tarehe 21 mwezi huu kundi hili litaporomosha show babu kubwa katika ukumbi wa Christian Foundation Center almaarufu CFC hapa jijini Nairobi na pia katika shule ya wasichana ya Njambini ministy.Tayari video kadhaa ziko nje na unaweza kuzitazama kwenye Yuo Tube-Nissi The Band Kenya pamoja na facebook.wakitumia jina lilo hilo.
Wengine katika Band hii ni pamoja na Wellei Gachau ambeye ni ndugu ya Jimmy Gachau,(Pacha)Pasqueline,Esther,Lilian Kimondo na Maggy.

Monday, 2 July 2012

JI KUTOA NGOMA MPYA

JI
Baada ya kukaa chini ya maji kwa muda mrefu msanii Juma Issa a.k.a JI mtoto ya Nzega kutoka Tanzania anakuja tena upya.
Kulingana na habari tulizo zipata kutoka Talent Entertainment ni kwamba msanii huyo aliyetoka na kibao Kidato Kimoja,tayari amereko vibao kadhaa katika studio hiyo.
Huku akiwa anasubiri kuzindua  rasmi vibao hivyo vikali,JI inasemekana kwamba amehamia humu nchini na kusemekana kujikita kabisa katika stuio hiyo mpya amabayo produza wake ni Elly Zee.
Vibao ambavyo atarelease hivi karibuni ni  Chukua kibao kikali sana pamoja na Dokta na vingine ambavyo atavitaja siku ya uzinduzi wake.
Mikakati tayari inafanywa ya kushoot wimbo Dokta katika Studio za Super Star Films nchini Uganda tarehe kumi na tano mwezi huu wa july.
Mbali na kutamba ni kibao Kidato Kimoja,pia alitoa vibao kama vile Katoto Kadogo.Kachuchu Mti wangu baadhi ya vingine vingi.

Wednesday, 27 June 2012

MR BLUE:MTOTO WANGU HATAKUWA MSANII

MR BLUE

 Endapo kweli mziki ungekuwa zaidi ya parapanda ya mwisho,basi mtoto Herry asingekubali kuondolewa kwenye fungu la wasanii wa kizazi kipya.
Mr.blue aka 'Kabayser' pamoja na mama watoto wake Wahida Mohamed wamesema mtoto wao kamwe akikua hawapendi afanye muziki kama yeye kwakuwa hawapendi awe maarufu.
"Mimi ningependa mwenyezi Mungu amjalie awe mtu fulani ambaye kidogo atakuwa hata kiongozi kusaidia watu,” alinena msanii huyo.
Hata hivyo blue amesema aliamua kumpa jina lake mwenyewe la ‘Herry’ kwasababu ni mtoto wake wa kwanza.
Haya tunamtakia herry juniour maisha mema hapa duniani.