![]() | |
MB DOG |
Baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye ramani ya muziki hatimaye msanii wa kizazi kipya Mb Dog amerudi kwa kishindo na kibao kipya kinachojulikana kama 'The Only One'.
Alitayarisha wimbo huo kwa studio yake mwenyewe aliyofungua hivi majuzi, Makopa inc.
Msanii huyo aliyetamba zamani na kibao 'Latifa' amesema kwa muda mrefu alikuwa akifanya mambo yake nchini Ujerumani na sasa ameamua kurudi rasmi kwenye muziki
Mb Dog anadai kuwa hana wasiwasi kuwa ataigusa tena nyoyo za mafaans wake wa Tanzania kwa kuwa haoni kipingamizi chochote na muziki hauja badilika sana.
Msanii huyo alidai kuwa kibao chake kipya kinaweza kuwa zaidi ya kile cha Latifa.
No comments:
Post a Comment