![]() |
JI |
Baada ya kukaa chini ya maji kwa muda mrefu msanii Juma Issa a.k.a JI mtoto ya Nzega kutoka Tanzania anakuja tena upya.
Kulingana na habari tulizo zipata kutoka Talent Entertainment ni kwamba msanii huyo aliyetoka na kibao Kidato Kimoja,tayari amereko vibao kadhaa katika studio hiyo.
Huku akiwa anasubiri kuzindua rasmi vibao hivyo vikali,JI inasemekana kwamba amehamia humu nchini na kusemekana kujikita kabisa katika stuio hiyo mpya amabayo produza wake ni Elly Zee.
Vibao ambavyo atarelease hivi karibuni ni Chukua kibao kikali sana pamoja na Dokta na vingine ambavyo atavitaja siku ya uzinduzi wake.
Mikakati tayari inafanywa ya kushoot wimbo Dokta katika Studio za Super Star Films nchini Uganda tarehe kumi na tano mwezi huu wa july.
Mbali na kutamba ni kibao Kidato Kimoja,pia alitoa vibao kama vile Katoto Kadogo.Kachuchu Mti wangu baadhi ya vingine vingi.
No comments:
Post a Comment