![]() |
AY |
Msanii kutoka bongo anayejulikana kama AY anatuarifu kuwa yeye huzunguka na bibilia yake alioachiwa na marehemu mama yake kila mahali aendako.
Msanii huyo wa kizazi kipya alisema mamake alimwachia biblia ambayo tangu akaabidhiwe mkononi hajawahi kuiacha kila anaposafiri kwenda mikoani ama nchi za nje kupiga show ama shughuli za kibinafsi basi biblia hiyo lazima iwemo kwenye begi lake. anasema hawezi lala kabla yeye kusoma vifungu kadhaa kutoka kwa bibilia hiyo hata ikiwa amepiga mitungi yake
Msanii huyo humfanyia ibada kanisani mamake kila wakati wa ukumbusho. anadai kuwa wakati mmoja siku hiyo muhimu ilimpata Moscow na ikawabidi watayarishi wake wa fanye juu chini ili kupata kanisa na AY afanye ibada hiyo.
Msanii huyo ameonyesha heshima na upendo mkubwa aliyokuwa nao kwa mamake mzazi
No comments:
Post a Comment