![]() |
NISSI THE BAND |
Kundi la Nissi The Band Kenya ni kundi linalokuja kwa kasi ki mziki wa injili katika miondoko ya kizazi kipya.
Kundi hili linaloongozwa na Jimmy Gachu aka J Moo limerekodi ngoma mpya inayojulikana "Moyo Wangu"katika studio za Talent Entertaiment chini ya produza Elly Zee hapa jijini Nairobi.
Katika hali ya kujizatiti kimziki,kundi hili limetoa album inayoitwa "Mabawa"iliyo na ngoma sita zikiwemo Baba Yangu,Mabawa,Mpenzi,nyingine zikiwa kwa lugha ya Kikuyu kama vile Ihua(Rose) na Makaya(Kilio).
Hata hivyo tarehe 21 mwezi huu kundi hili litaporomosha show babu kubwa katika ukumbi wa Christian Foundation Center almaarufu CFC hapa jijini Nairobi na pia katika shule ya wasichana ya Njambini ministy.Tayari video kadhaa ziko nje na unaweza kuzitazama kwenye Yuo Tube-Nissi The Band Kenya pamoja na facebook.wakitumia jina lilo hilo.
Wengine katika Band hii ni pamoja na Wellei Gachau ambeye ni ndugu ya Jimmy Gachau,(Pacha)Pasqueline,Esther,Lilian Kimondo na Maggy.
No comments:
Post a Comment