Wednesday, 13 June 2012

NYOTA AVUMISHWA KUFA

NYOTA NDOGO
Uvumi wa kifo cha msanii Nyota ndogo,umeshtua wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini.
Hii nikufuatia mtu asiyejulikana kuazisha tetesi hiyo kupitia mtandao wa facebook.
Habari zinzotufikia katika meza yetu ya Ketau Express ni kwamba mtu  huyo asiyejulikana alieneza habari hii pasi na Nyota Ndogo mwenyewe kujua.
"Nilishtuka kusikia ati nimekufa"alisema nyota akiwa na mshtuko mkubwa moyoni."Nilipigiwa simu na watu wengi ikiwemo familia yangu wakihofia tetesi hii iliyosambaa"aliendelea kusema msanii huyo.
Wakati wa tukio hilo msanii huyo alikuwa hapa jijini kwa kazi zake za kimziki na kazi nyenginezo.Ama kwa kweli inasikitisha sana mtu kukaa na kubuni uvumi kama huo.Hata hivyo udashadash wetu iligundua ni uvimi tu.

No comments:

Post a Comment