![]() |
CHIDI BENZ |
Wasanii wawili wakali kutoka Tanzania wakiongozwa na nyota wa kizazi kipya,Abdhalla Mwakwiro aka chidi na Albert Mangwea wameunganisha vichwa vyao na kuingia studio tayari kwa kollabo na tayari wameshaingiza sauti zao katika wimbo huo.
Wimbo unaojulikana ''House Paty''unatajiwa kuwa wimbo mkali tena matata kutokana na kushirikiana na wasanii hao ambao wanajulikana kwa staili zao tofuati katika mziki wa kizazi kipya.
![]() |
NGWAIR |
Wadadisi wanasema kwamba msanii Mangwea yupo imara tena baada ya kimya kirefu na anatarajia kufunika mistari ya wimbo huo na hana budi kurudisha hadhi yake ya zamani.
Wasanii wengine kwenye wimbo huo ni mwana dada Coreen
Mwamani ‘Sindi na Godzilla.‘House Part’ unatengenezwa na mtaalamu Lamar Niekamp maarufu kama
Lamar wa Lamar, ndani ya Studio yake iliyopo mtaa wa kariaoko Tanzania.
Mbali na kufanya wimbo wa pamoja kama mambo yakienda vizuri wamepanga
kutengeneza albamu ya pamoja, ambayo wanaamini ikikamilika itakuwa ni
moto wa kuotea mbali kutokana na vichwa hivyo kushiriki.
No comments:
Post a Comment