Tuesday, 26 June 2012

MACHOZI KUISHI KENYA

Hussein Machozi
Huenda Hussein Machozi msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania kuhamia Kenya. Kulingana na taarifa ya waliokaribu na msanii huyo wanasema kuwa,  huenda  akawa na makao humu nchini  kwa sababu miziki yake inakubalika zaidi kuliko Tanzania ambako msanii huyu anatokea. 
Karibuni Hussein Machozi ameonekana katika studio ya Talent Entertainment iliyoko maeneo ya Burubru  chini ya producer Elly Zee kurekodi ngoma kadhaa ikiwemo kolabo aliomshirikisha msanii Size 8 wimbo unaojulikana Nipe na Addicted aliyoimba pekee. 
Pia vile vile Machozi tayari amefanya kolabo na wasanii Fat S aka Salim Mwinyi na Mohammed Mwamba almaarufu Fisherman kutoka Mombasa
Wimbo Addicted ni wimbo uliyo na ujumbe kwa mabinti na video yake imefanywa na studio za Ogopa .  

No comments:

Post a Comment