![]() |
DNA |
Baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miaka mitatu, msanii aliyetamba na kibao Banjuka DNA amewashangaza mashabiki wake kwa kurudi tena katika mziki wa Secular. Hii ni baada ya msanii huyo kujikita katika mziki wa injili.
Kwa kweli ni jambo la kushangaza kwani DNA kwa sasa amejitokeza tena na kutoa kibao kipya kwa jina "Maswali ya Polisi"na amewaambia mashabiki wake kuwa yeye si msanii wa injili.
Ketau Express ikiongea na mshirika wake wa karibu ambaye ni Yusuf Noah a.k.a Refigah ambaye pia ni promoter mkubwa nchini, alisema DNA amerudi katika mziki wa kizazi kipya baada ya panda shuka nyingi ya maisha."Nilimshawishi DNA ili abadilishe style yake ya mziki na alikubali", alisema Refigah.
Kwa upande wake msanii DNA alikiri kuwa mziki wa Secular ndio unamuuza na kupata mapato akilinganisha na mziki wa injili."Niliamua kurudi kama zamani kwa sababu niliona mashabiki wangu bado wananijua na wananihitaji, kwa hivyo kurudi kwangu katika mziki wa Secular nimeona ni uamuzi wa busara na namshukuru sana mweledi wangu Refigah kwa kunishauri, na kwa mafans wangu wasishutuke. Maswali ya Polisi ndio wimbo nawapa".
Wimbo huo umefanyiwa kazi katika studio za Grandpa Records.
No comments:
Post a Comment