Tuesday, 19 June 2012

AY ATOA PARTY ZONE RASMI

AY
Video ya wimbo "Party Zone" ya msanii mkali wa bongo AY ambayo imekuwa ikisubiriwa sana na mashabiki wake kule nchini Tanzania sasa imekamilika na ishatoka rasmi.
Video hiyo ambayo msanii AY kamshirikisha Marco Chali,inakisiwa kutumia maelfu ya hela na hivi sasa inafukuziwa na kila stesheni ya runinga nchini humo mpaka vituo vya kigeni tayari imeonyesha video hiyo kali.Uwezo wa video hiyo kwa kweli ni kali sana.
Party zone ni zile nyimbo ambazo huingia kichwani kwa mtu haraka na kujikuta akiuimba kimya kimya bila kuwa na taarifa.
Ngoma hii imetoka katika kipindi ambacho nyimbo za aina hii ya dance zinafanya vizuri mno duniani. Ni wimbo wa biashara zaidi na tuna uhakika utampeleka mbali sana.

No comments:

Post a Comment