Wednesday, 9 May 2012

KUWENI MACHO WASANII

RICHIE ONE
Aliyekuwa wakati mmoja  member wa kundi la TMK Wanaume Halisi Rich One, anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Msimbazi kwa kosa la kutumia jina la Ali Kiba kuwatapeli mapromota mbali mbali.
Msanii huyo anadaiwa ku-divert simu zinazopigwa kwa namba ya Ali Kiba na kuzipeleka katika simu yake, baada ya hapo anakubaliana na mapromota kufanya show na kupokea advance kwa kuwapa namba yake ya mpesa. Siku ya show promota anajikuta katika wakati mgumu baada ya kutomuona Ali Kiba.
Meneja wa Ali Kiba, Frank Gonga amethibisha kukamatwa kwa Rich One na kwa kweli imekuwa mchezo kwa mapromota na watu binafsi kufanya mchezo huo ambao umewakandamiza wasanii wengi.hapa ketau Express haturuhusu jambo hili liwatokee wasanii kwani twakuza vipaji na tuana watahadharisha wasanii kuwa wawe macho kwa mapromota feki.

No comments:

Post a Comment