Wednesday, 2 May 2012

ELLY AWAKILISHA TALENT ENTERTAINMENT

ELLY ZEE
Unapozungumzia usanii kwa kawaidautafikiria kuhusu msanii mwenyewe,lakini huwezi kutambua aliyefanikisha kazi hiyo.Hapa nazungumzia kuhusu kazi ambazo produza mkali nchini anazofanya kwa ustadi.
Elly zee ambaye anashikilia Studio ya Talent Entrainment iliyoko hapa jijini katika maeneo ya Buruburu,ni produza aliye na kipaji kikubwa na kazi anazofanya zimekubalika afrika mashariki.Studio ambayo anaishikilia kwa sasa na ambayo ni mpya kabisa jijini, ni studio ambayo meza ya Ketau Express imebaini kwamba kali ilipotembelea.

Studio hiyo iliyojengwa kwa mamilioni  ya pesa imewaleta wasanii kutoka Bongo amabao ni JI aka mtoto wa Nzega pamoja na msanii Sir Godizzo msanii chipukizi anayekuja kwa kasi katika sanaa ya mziki wa kizazi kipy.
PRODUCER ELLY ZEE STUDIONI
Akiongea na meza ya Ketau Express produza Elly Zee alisema kwamba kuna wasanii wengine ambao wanafanya kazi pamoja lakini cha msingi ni studio kupata hadhi ya juu na kujulikana."ningependa kufafanua kwa wasanii wote kwamba wanaweza kuja kurecord hapa na ukizangatia studio ni ya kisasa na vile vile bei yetu ni rahisi"alisema Zee.Wenngine ambao wamechangia ufanisi wa studio hii ni pamoja Vincent almaarufu Vinnie na Dennis aka Deno ambao ni wafanyibiashara wakubwa hapa jijini. 



No comments:

Post a Comment