Friday, 20 April 2012

MR NICE KUTOA KIBAO KINGINE

Mwasisi wa densi ya TAKEU nchini tanzania, Mr Nice ameonyesha hadharani kuwa bado yu mkali katika ukumbi wa miziki ya kizazi kipya.

Nice ameweka wazi kuwa wiki ijayo atakuwa anaangusha kitu kipya hii ni baada ya wimbo wake unaozidi kufanya vizuri Afrika Mashariki "Tabia gani"
 "wiki ijayo mimi ntawapa kitu kipya mziki ulioenda shule na fleva tofauti kabisa" alinukuliwa akisema msanii Mr Nice.
Ngoma hii mpya ya Mr Nice akiwa ameshirikiana na Mkali wa Bongo fleva afrika mashariki Naseeb Abdul aka "Diamond" itajulikana kama "NIONJE".
wimbo huu umefanywa nchini ya producer Lamar wa Fish Crab Studios, na huu utakuwa wimbo wa pili wa Mr Nice kwenye album yake inayojulikana kama "Tabia Gani" anayo ishughulikia kwa sasa.

Bila shaka Ketau Express itakuletea wimbo huu live punde tu Mr Nice atakapoizindua rasmi.

No comments:

Post a Comment