![]() |
DIAMOND |
Baada ya matarajio ya wengi kutazamia msanii wa kizazi kipya kutoka bongo Diamond kutangaza wazi uhusiano wake na mchumbawe wa muda mrefu,sasa jibu lao limejibiwa kikamilifu.
Diamond, kupitia mtandao wake wa facebook amekiri kumpenda Jokate kwa kuweka picha yake na kuambatanisha status message iliyosema,“I love you Kate and there is no one like u in ma life”Inasemekana kwamba Diamond na Jokate walianza uhusiano wao wakati Diamond bado akiwa anatoka na Wema Sepetu ambapo ikampelekea Wema kumtaja Jokate kwenye vyombva vya habari kwamba ndiye anayemharibia uhusiano wake na Platnumz.
Wawili hao walikana uhusiano wao mara kwa mara, ingawa ishara zote zilionyesha ukweli wao na kwa kua mapenzi ni kikohozi na kulificha huliwezi, hatimaye penzi limefichuka.
Kuambatana na hilo msanii Diamond ,aliwahi kufanya video na Kate, ya wimbo wake wa ‘Mawazo’Meza ya Ketau Express inamtakia Diamond maisha mema kimapenzi.
No comments:
Post a Comment