Thursday, 19 April 2012

DAVIES AWA MGENI WA SERIKALI CENTRAL

 Aliyekuwa mshindi wa Tusker Project Fame, Davis Ntare juzi alikuwa mgeni wa serikali hapo na jana alifikishwa korokoroni katika stesheni ya Central.

Kulingana na habari zinazofikia meza yetu ya ketau Express ni kuwa mshindi huyu wa milioni 5 alikamatwa siku ya jumanne usiku katika pub ya Tribeca kiungani mwa mji wa Nairobi baada ya kuzua rabsha na walinzi wa kilabu hio.

Rabsha ilizuka pale msanii huyu alipomuuma kidole cha gumba mwanamke mmoja anayejulikana kama Maryanne Karanja jambo lililosababisha kukamatwa kwa star huyu ambaye hivi sasa anajulikana na mziki wake unaojulikana kama "sheka sheka".

Kufikia sasa bado hatujabainisha kilicho sababisha msanii huyu kumtendea mwanadada Maryanne Karanja ukatili huu.

No comments:

Post a Comment