![]() |
| MOG |
Licha ya kuwa mafans wao walifurika kwa wingi ndani ya ukumbi huo wasanii hawa we kipaji cha kipekee waliwashangaza wengi walipodinda kupiga show na kusababibisha hali ya taharuki na hasira kwa mafans wao.
Huku chazo hasa cha MOG kususia show hio ni kuwa hawakuwa wamelipwa hela ambazo walikuwa wameagana na promoter we event hio.Pormoter huyo ambaye ni mzaliwa wa Kenya anayeishi Dubai na anafahamika kama Hassan Waziri alikuwa amewaahidi MOG nusu ya pesa za makubaliano yao kabla ya kuabiri ndege hadi Dubai na masalio,wapate kabla ya kupiga show, lakini promoter huyu hakufanya hivyo.
Jambo hili lilizua hali ya taharuki ukumbini baada ya MOG kudinda kupiga show huku mafans waliokuja kwa show hio wakidao pesa zao na walisaidiwa na maafisa wa polisi waliokuwa katika eneo hilo.
Uchunguzi wa onesha kuwa promoter huyu sampli ya kaka Saidi amewahada wasanii kadha toka Kenya wakiwemo P – Unit, Mike Rua, Bigpin, Dj Kaydee, Kriss Darling, Kidum na Creme De La Creme.

No comments:
Post a Comment