![]() |
NYOTA NDOGO |
Nyota ambaye alivuma na vibao kama vile 'Watu na Viatu', 'Hao' na vingine vingi alisema hakujua moto wenyewe ulitokea wapi alishtuka kuona majirani wakiuzima moto huo."sikuelewa kilichosababisha moto huu kutokea lakini nashukuru majirani zangu kwa kuuzima moto ambao ungeteketeza nyumba yangu yote".
Nyota alijenga nyumba hiyo miaka michache iliyopita katika mji wa Voi baada ya kuuhama mji wa Mombasa na kupata kipande cha aridhi alichonunua yeye mwenyewe.
Hata hivyo wakati wa tukio hilo msanii huyu hakuwa karibu kwani alikuwa jijini nairobi kufanya kolabo na msanii Karen Lucas aka Kaz, na kufikia sasa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
No comments:
Post a Comment