![]() |
| KIDUM |
Msanii Kidum kutoka nchini Burundi ambaye anafanyia kazi zake za
muziki humu nchini Kenya na ambaye amefanikiwa kufanya vyema hapa Afrika
Mashariki kutokana na nyimbo zake,kama vile Mapenzi,Greedy ,Abambuzi haturudi nyuma aliyomshirikisha msanii Juliana kanyamozi kutoka Uganda,anatarajiwa kugonga bonge moja la
show akiwa pamoja na Peter Msechu kutoka kule Tanzania.
Show hiyo iliyopangwa kufanyika 'Mbalamwezi Beach', inatarajia kufanyika Ijumaa ya Mei 4 mwaka huu.
Kidumu ambaye alikuwa kioo kwa msanii Peter Msechu wakati wa
shindano la Tusker Project Fame, atasindikizwa na msanii huyo katika
nyimbo zake atakazoziimba usiku huo.

No comments:
Post a Comment