Msanii wa kike anayekuja kwa kasi katika mziki wa kizazi kipya nchini anayefahamika kama Sossun ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake Get Wested sasa ameufanyia wimbo huo video kali.
Wimbo huo ambao umekuwa nje kwa miezi michache tangu kutoka kwa audio yake,umekuwa ukifanya vyema sana kwenye stesheni mbalimbali za radio nchini.
Akiongea na meza ya ketau express kupita mtandao wake wa facebook aliezea shukrani zake kwa mashabiki wake ambao kwa sasa wamemkubali kimziki na ambao wanaendelea kumpa shavu kwa kila njia.
Sossun ambaye jina lake linamaanisha SO SOON ni msanii ambaye hufanya rap za nguvu katika mchanganyiko wa style za Ghipuka yaani Genge
HipHop na Kapuka!!
hata hivyo msanii huyu wa kike akiwa chini ya studio ya Pacho Entertainment china ya producer Rapdamu asema mambo mengi makubwa yanakuja huku video ya ya wimbo Get Wested ikiwa imefanywa na studio za Boomba chini ya producer Thome.
No comments:
Post a Comment