Tuesday, 10 April 2012

KAMBUA AFUNGA PINGU ZA MAISHA

 Jumamosi iliyopita, msanii wa nyimbo za kidini, Kambua Manundu alifunga pingu zake za maisha na Jackson Mathu ambaye ni mhubiri na vilevile ni mwanabiashara, katika bustani  ya Windsor Golf Hotel ambayo hujulikana sana kuwa na mazingira ya kupendeza ambayo hutumika sana kuendeleza sherehe za harusi.
Kambua pamoja na bwanake Jackson walikaribishwa jukwaani ambako walijiburudisha kwa nyimbo kadhaa za kundi la wanamuziki  linalojulikana kama Kayamba Afrika.
Baadhi ya wasanii waliowaburudisha watu kwa nyimbo zao walikuwa Esther Wahome, Mercy Masika na Marsha Mapenzi.
Kati ya wageni walioalikwa kuhudhulia harusi hiyo ni wasanii Alice Kamande, Nancy Kihenia na SK Blue, daktari Amrit Kalsi na Churchil ambaye ni mwigizaji.





No comments:

Post a Comment