Hivi sasa nchini uganda mambo si mazuri kwa msanii Bebe
Cool ambaye hivi sasa anasakwa na Bi Constance kwa madai ya kuto lipa kodi yake nyumba alipokuwa anaishi katika mtaa wa kifahari wa Kiwatule. Bebe Cool ambaye amekuwa kwenye chati nyingi afrika mashariki na nyimbo zake kama vile Kaspeki na Minzani.Alikuwa mkaazi wa nyumba anayodaiwa kodi mwaka 2009.Inakisiwa kuwa kodi ya nyumba ya Bebe Cool kwa mwezi iligharimu laki 700.
Na baada ya mwaka mmoja msani Bebe Cool alifurushwa kwenye nyumba hio inayomilikiwa na Bi Constance aliposhindwa kulipa kodi ya miezi sita mtawalia.
kuzidisha ni kuwa Msanii huyu alikuwa na deni kubwa la umeme bill lililo gharimu millioni 3 na nyinginezo kama vile maji ambazo inakisiwa hakuwa amezilipa.
Jambo hili lilimkera sana Bi Constance ambaye aliamua kutafuta usaidizi toka kwa waziri wa zamani aberi Bidandi Sali ambaye ni babake Bebe Cool.Lakini babake Bebe Cool alikwepa swala hilo akisema kuwa Bebe ni kijana aliyebalehe na anafanya jazi basi anauwezo wa kulipa madeni yake.
No comments:
Post a Comment