![]() |
susumila |
Wimbo "Si vibaya" wa msanii Abdhalla Suleiman aka Chikuze ambao unafanya vizuri Afrika Mashariki umeleta utata kwa mafans ambao wanauona kwamba wimbo umetolewa kwa beat ya wimbo "Mwanzo mpya" wa msanii Susumila.
Hii ni kutokana umoja wa beat hiyo sambamba na vile nyimbo zote mbili zilivyopokelewa. Ketau Express ikiongea na Susumila, alikiri kwamba utata wenywe unasemekana upo lakini upande wake alisema hana shida na hilo.
"Ni kweli kwamba rumours zipo na sielewi kwanini watu wanazungumzia hilo.kwangu na heshimu kazi zangu na za wasanii wengine"
Upande wake Chikuzee alisema kwamba hamna haja ya kulizungumzia swala hilo kwani ana heshimu kazi ambayo huifanya kulingana na mwelekeo wa producer wake.
"Sielewi mafans wanahitaji ninni lakini uwezo wangu kimziki haulinganishwi na kazi za watu wengine ambao pia na heshimu kazi wanazofanya"
Tukiachana na ubishi huo Susumila ambaye awali amevuma sana na wimbo wake "Kijana jipange" aliomshirikisha mgenge mejja ametoa wimbo mwingine mpya unaojulikana "Mikwanja" ambao ameshirikisha msanii wa mombasani Kibzzo.
Msanii chikuzee naye hivi karibuni amebadilisha mtindo wa kuimba kutokana na kile anachosema kuwa baadhi ya wasanii wachanga mjini mombasa wanatumia sauti yake ili kupanda chati.ukisikiliza wimbo"Si vibaya" utasikia flava tofauti na amesema kuwa ataendelea vivyo hivyo na anatarajia kutoa ngoma yake mpya kwa jina Mapenzi.

No comments:
Post a Comment