Wednesday, 22 February 2012

CHAT NA WAHU FACEBOOK!!

NAMELESS & BABY TUMISO
Wikendi iliyopita mwanamziki Wahu aliyenoga na kibao Sweet Love, aliwashangaza mashabiki wake alipokubali kuchat nao moja kwa moja kwenye ukurasa wake wa Facebook 'Wahu Kagwi', jambo ambalo 'celeb' hawajawahifanya. Mashabiki walimuuliza maswala ya mwanawe, mumewe Nameless ambaye ni mwanamziki na kuwa mzazi.

Alijibu maswala yote na kusema kuwa mwanawe yuko shule ya chekechea na mwaka ujao atakuwa darasa la kwanza.Alipoulizwa kama anampango wa kupata mtoto mwingine alijibu "ako kwa jam anakam" Alikana uvumi kuwa ndoa yake inamisukosuko na kuwakanya mashabiki wake kuamini uvumi.

WAHU
Mazungumzo     yaliendelea kwa zaidi ya saa moja huku ma'fans wakimshukuru kwa unyenyekevu wake. mwanamziki huyu alizindua kibao Still a Liar, unaosisitiza maudhui ya wimbo Liar alichoimba miaka ya hapo awali. Kibao hiki kinavuma mitamboni kwa sasa!!

No comments:

Post a Comment