Friday, 10 February 2012

ROSE MUHANDO BALOZI WA SONY

Kampuni ya bidhaa za Sony Barani Afrika kupitia vifaa vyake vya muziki imemteua mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Rose Muhando, kuwa mmoja wa mabalozi wake.Rose Muhando amepata shavu kubwa ikiwa ni dili ya kurekodi miziki na kampuni heavyweight duniani ya muziki ya Sony. Alimshukuru Mungu kwa kumpa nafasi hiyo ya kipekee, na kuwashukuru waliomuwezesha kimuziki miaka mingi ya yeye kuwepo kwenye industry.

Uteuzi huo umetangazwa leo (10/02/2012) na Mkurugenzi wa Mambo ya Masoko, Manusha Sarawan, katika mkutano na wanahabari uliofanyika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Manusha alisema mchakato wa kumpata balozi huyo   ulishirikisha wanamuziki wakongwe zaidi ya 130 barani hapa. Muhando anayejulikana kwa nyimbo zake kama Nibebe, Utamu wa Yesu zinazo tumika kama ringtones na wengi Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment