Friday, 10 February 2012

DONDA LILOSABABISHWA NA DINI

Zimesalia siku nne tu kabla ya kusherehekea siku ya wapendanao ama ukipenda Valentines Day. Katika pitapita zetu kama wanaKETAU Express ilikukupa udashdash wa wasanii kwa matayarisho ya siku hii inapowadia.

Marya na Mustapha ni mojawapo ya wasanii ambao walikuwa pamoja lakini tofauti zao za kidini hazikuwaruhusu kuwa pamoja kama mme na mke.

Miezi michache baada ya kutengana Mustapha alimtungia Marya wimbo "Mena Pyaar Kiya"-Nimependa, pamoja na msanii wa kiindi Alisha Popat.

Wawili hawa wameonekana pamoja kwenye Ogopa video shoot wakiwa na furaha na hata kuketi pamoja isiyokuwa kawaida yao baada ya kutengana.
Marya alisema wazi kuwa wimbo aliotungiwa na Mustafa ni wa dhamana kwake na mwanamziki huyo ni mfano bora wa mwaume yeye angependa kuolewa naye. Mustapha pia alikiri kumpenda Marya lakini anajifunza kuishi bila yeye. Mabo ni kama hayo msimu huu wa Valentines..





No comments:

Post a Comment