
Baada ya kimya kirefu, msanii Ronny B aka Funga Ukanda aliyeimba vibao Mr.Onyango, Niridhike,
Ichanda Nang'o( Wanisumbulia nini) amejitokeza tena lakini sio kwa maswala ya mziki. Tangu mwaka jana kuna jambo ambalo limemmkosesha usingizi na imebidi aliseme mbele ya washika dau wake akihusisha blog yetu (KETAU Express) Ronny B ambaye anasema kwamba amekuwa akipata sms za vitisho kutoka kwa mtu asiyemfahamu. "Jamaa huyo adai kwamba nina uhusiano wa kimapenzi na mpenziwe." Jambo ambalo B anakana. !Mimi huyu jamaa simjui na sijawahi kumuona anayosema siyajui."
Baada ya kujulisha watu wake wa karibu B amechukua jukumu la kupeleka jumbe hizo katika kituo cha Polisi kuandikisha taarifa kwa Idara ya Upelelezi. Tayari hatua imechukuliwa.
KETAU Express imedhibitisha kuwa msanii Ronny B alipata jumbe hizo.
No comments:
Post a Comment