Monday, 27 February 2012

LADY CONNY AVUNJA KIMYA CHAKE

LADY CONNY
Mwaka 2009 alipotoa kibao "sikuhitaji tena" alichomshirikisha msanii fisherman, badaye alizuka tena na kibao "Natambanae" ambacho pia amemshirikisha msanii huyo huyo pia kushirikishwa na mwanadada mwenzake kutoka Ujerumani kwa jina Mama Sizo msanii mwanadada kutoka mombasa anayefanya vizuri sana Afrika Mashariki. Lady Conny amekiri miziki yake miwili ya kwanza imeletwa na hisia za kimapenzi. wimbo sikuhitaji tena unazungumzia vile alivyoteswa kimapenzi na hataki tena dharau za mwanaume aliyemwamini. 

Wimbo Natambanae ni ufuatilizi wa wimbo wa kwanza ambapo anazungumzia kuhusu  mchumba aliyempata na ameridhika kiroho.

KETAU Expresss ilipomuuliza ikiwa anamchumba alisema "Yes yupo na siwezi jifanya kuwa sina boyfriend. Maisha hubadilika na mimi ni mwanadamu hisia ninazo kama mabinti wengine.Awali nilichukia sana kufanya urafiki na mwanaume lakini maisha lazima yaendelee." Msanii huyu amefanya ngoma zake katika studio ya Mwamba Records ilioko kusini mwa mji wa mombasa chini ya producer  Nuru, amesema pia mwaka huu atafanya kazi na wasanii wengine na kazi kubwa inakuja ingawaje hakutaka kusema ni wasanii gani atafanya kazi nao.

No comments:

Post a Comment