![]() |
Rojo-Mo |
Baada ya kutoa wimbo wake mpya wiki tatu zilizopita msanii Rojo-Mo kutoka Mombasa amevunja kimya chake na kuelezea wimbo wenyewe vile unamaanisha ilikutoa utata wakijamii katika eneo la pwani. hii ni kutokana na tashwishi uliozunguka wimbo wenyewe.
wimbo "Vampire" ndio jina. katika wimbo huu Msanii Rojo-Mo anaelezea mambo ya kutisha lakini hii ni kinyume na vile mambo yalivyo katika sehemu ya Pwani."Nimeimba wimbo huu ilikutahadharisha jamii kuhusiana na ushetani ulioko Pwani. na hii ni dhana ambayo watu wengi wako nayo kuhusiana na majini.
Hata hivyo dhana hiyo imechukuliwa vyema na Mziki wenyewe sasa hivi unafanya vyema katika stesheni mbalimbali za radio nchini ikiwemo Ketau Express. wimbo huu amemshirikisha msanii Sudi Boy na umefanyiwa katika studio za SQ records Mombasa na Video ipo njiani.
No comments:
Post a Comment