![]() |
| Juma Nature |
Baada ya kimya cha muda mrefu Juma Kassim aka Nature aka Qibla ameibuka na kudai
mwaka huu ni wake na anataka kurejesha heshima ya miziki wake.
Nature ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi amesema kundi hilo
limekamilisha albamu yao ambayo wataitaja miezi michache ijayo, lakini
baadhi ya nyimbo tayari zipo redioni zikifanya vizuri.
Nature alisema kwamba album hiyo imewashirikisha wasanii kama vile Dollo, Richie One, JB aliyekuwa
Mabaga Fresh, Bob Q, D. Chief, Malipo, Kaka Man, Mzimu na Eddo.
Nyimbo ambazo tayari zimekamilika ni 'TMK', 'Able' na 'Mguu nje Mguu
ndani remix' ambapo kazi kubwa imefanywa na Dolo, KR Mullah na JB. Album hiyo pia imefanywa katika studio yake binafsi ambayo ni Halisi Studio.

No comments:
Post a Comment