| MR. BLUE |
Msanii anayebobea kwa nyimbo za rap kutoka Tanzania, Kherry Sammer Rajab aka Mr. Blue, amuonyesha kidole cha lawama msanii chipukizi Raz, kwa kuiga jina lake kwenye ukurasa wa Facebook. Micharazo jina ambalo Rama Sultani aka Raz Micharazo hutumia kwa muziki wake lasekana kutumiwa kimajazi na wasanii wengine kama vile CLD,Bobby Mapesa na watanzania kadhaa akiwemo Mr. Blue.
Msanii CLD na Raz ni mabinamu na hio kufanya Mr. Blue kumdhania yeye ndiye anaiga jina hilo kwa Facebook na kujipatia hela kutoka kwa mabinti rafiki zake.
Msanii huyu anayejulikana kwa kibao chake We ni Wangu, alichomshirikisha Belle, alidaikuwa atamripoti Raz kwa polisi iwapo hataacha kuiga jina lake.
Raz alisema kuwa anawaheshimu wasanii wote na anajiweza kifedha kujikimu mwenyewe. aliongezea kusema kuwa huo ulikuwa uvumi wa watu wakatili wa Mombasa wanaotaka kuharibu uhusiano wake na wasanii wengine.

No comments:
Post a Comment