![]() |
BAGHDADI |
Baghdadi mmoja wa wasanii wa kundi la Mexicana Lacavela hapo jana alitangaza rasmi kujitoa
katika kundi hilo alilolianzisha karibia miaka miwili iliyopita.
Rapper huyu alisema kwamba ameamua kuachana na kundi hilo
ili aweze kusimama na kazi zake binafsi baada ya kumpata manager
atakayemsaidia kufanikisha malengo yake. Sababu nyingine aliotaja ni kutokuelewana na wenzake katika ratiba za
kikazi na wanapopanga kukutana na wenzake.
Kundi hili linajulikana na kibao chao Kamba 2 Kamba bila shaka watanoa makali yao ilikuweza kufufua kundi hili kimziki.
No comments:
Post a Comment