Msanii aliyewahi kutamba na kibao cha ‘Bullet’, Quick Racka, amesema kuwa ngoma yake mpya ambayo itafungua ukurasa mwaka huu wa 2012 ni ‘Fire Anthem’, ambayo inatarajia kutoka muda wowote kuanzia sasa.
Akifunguka msanii huyo alisema wimbo huo ameufanyia katika studio za MJ chini ya Marco Chali, ambapo anaamini ngoma itafanya vizuri kwani amefanya kitu ambacho ni tofauti na watu walivyozoea.
Alisema kabla ngoma hiyo haijawa sokoni anahitaji kutengeneza video yake ili mashabiki wake wapate burudani sehemu zote sambamba na Audio.
“Fire Anthem, ni ngoma ambayo haina mfano hivyo natumai muda wowote nikishatengeneza video kazi itakuwa hewani hivyo mashabiki wangu wategemee kuona utofauti mkubwa sana kutoka kwangu,” alisema.
No comments:
Post a Comment