Friday, 3 February 2012

Nyota Azidi Kung'aa

Baada ya kimya kirefu katika ulingo wa muziki,  Mwanaisha Abdallah aka Nyota Ndogo sasa amekuja upya. Hii ni baada ya yeye kutoa kibao kipya kinajulikana kama "Moyo."

Nyota ambaye yupo hapa jijini amefafanua kuwa mziki huu ameutoa ili kuvunja kimya chake kwa mashabiki ambao walimkosa kwa siku nyingi. 

"Nimekuwa nimenyamaza na sasa nimevunja kimya changu kwa kutoa wimbo huu "Moyo"   

wimbo wenyewe unazungumzia kuhusu mapenzi na kufafanua zaidi kwamba moyo huwahaujui dhiki kwani ukishapenda haujui kuumizwa kwa hivyo inabidi uzuie hisia ndio usiumie zaidi. 

wimbo huu umefanyiwa kazi chini ya producer Totti kutoka Mombasa na video ipo njiani. Sasa hivi inafanyiwa "editing." Hongera Nyota kwa kazi nzuri tuko hapa kukutetea!


No comments:

Post a Comment