Msanii wa kike wa kizazi kipya ambaye anakuja kwa kasi, Gin Ideal, amerelease wimbo mpya unajulikana kama "Want u Now", ambao unazungumzia maswala ya mapenzi.
Akizungumza na meza ya Ketau Express Ideal alielezea hisia zake ambazo zilimfanya atoe wimbo wenyewe
"wimbo wenyewe ni hisia yangu binafsi na nimelingaisha uhusiano wa mapenzi kwa mtu unayempenda na unakuta mtu mwenyewe hayupo katika maisha yako."
Tulipomuuliza zaidi kuhusiana na wimbo wenyewe alisema kwamba ni jambo lishawahi mtendekea na amewahimiza wanadada wenzake wasijiingize katika mapenzi kiholela.
Wimbo wenyewe umefanywa katika studio za Pacho Entertainment chini ya producer V6 na video tayari ipo nje. Kwa maelezo zaidi gonga juu uone Video yenyewe.
No comments:
Post a Comment