Thursday, 23 February 2012

'NIDANGANYE' WA SHETTA NA DIAMOND


SHETTA
DIAMOND
Baada ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Mdananda’, msanii Shetta, anatarajia kuachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Nidanganye’, akimshirikisha Diamond kipenzi cha warembo. Shetta alisema kuwa kazi hiyo itakuwa moto mkali kwani anaamini baada ya kushika soko na ngoma yake iliyovuma afrika Mashariki  hiyo itakuwa zaidi.

Alisema kuwa ameamua kumshirikisha
Diamond, katika wimbo huo ni kutokana na uwezo mkubwa aliokuwanao hivyo anaamini sauti yake itaweza kuifanya ngoma hiyo kulikamata soko kikamilifu. Aliongeza kuwa baada ya mchakato wa wimbo huo, atakuwa katika maandalizi ya albamu yake ya pili ambayo bado hajaipa jina huku akiaamini itafanya vizuri.

Kwa sasa nipo katika hatua za mwisho wa kumalizia ngoma yangu, hivyo nawaomba mashabiki wangu wakae tayari kuipokea,”
alisema.

No comments:

Post a Comment