Saturday, 25 February 2012

MR BLUE AACHA KUIMBA


MR BLUE
Msanii Mr. Blue a.k.a byser, anawashangaza mashabiki wake wikiendi hii baada ya kudai kuwa yuko kwenye michakato ya kubadilisha style ya muziki anayofanya kutoka kuimba mpaka kurap.
Kwa mujibu wa msanii huyu anayefanya vizuri kimziki Afrika Mashariki, anatamani sana kurudi kwenye style yake ya zamani ambayo ndiyo iliyomtoa kunako ulimwengu wa muziki.
Katika kudhihirisha kuwa hatanii, kuna wimbo mpya ambao anaratajia kuutoa hivi karibuni ambao utaonesha jinsi alivyobadilika.
Akihojiwa alisema, “Sihitaji kuimba kwasasa kwasababu najua style ambayo awali iliniweka juu kwenye chart,mashabiki wangu wataona utofauti wangu katika ngoma mpya ambayo itakuwa hewani hivi karibuni."

No comments:

Post a Comment