Saturday, 25 February 2012

ALBUM YA MWAKA HUU NJIANI

Msanii Quick Racka anayekuja kwa kasi  kutoka Tanzania,amesema anajipanga kuhakikisha anachomoka na albam yake ya kwanza mwaka huu ili iweze kuwa zawadi kwa mashabiki wake.
Racka alisema kuwa hata hivyo kwa sasa yupo katika mchakato wa kurekodi nyimbo zake tatu ambazo hajazipa majina ambazo zitakuwa sokoni baada kukamilikia.
Akiongelea wazo Racka alisema “Nafikiria kuachilia albamu mwaka huu, lakini bado sijajua itakuwa na nyimbo ngapi kwa sababu lengo langu kubwa ni kutoa ngoma moja moja, hivyo endapo nitajipanga vizuri basi albamu itakuwepo mwaka huu,” alisema.

Bila shaka KETAU Express twangojea vibao hivyo na albamu hii. Unaweza soma QUICK RACKA KUTOA "FIRE ANTHEM"

No comments:

Post a Comment