Wednesday, 8 February 2012

"Kamili Gado" Video ya Professor J Jikoni

Jana (08/02/2012)  mwanamziki Joseph Haule aka Professor Jay ama the Heavy Weight MC aliwaalika wanamitindo kibao kwaajili ya kurekodi nao video yake ya wimbo mpya uitwao "Kamili Gado." 

wimbo huu ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri sana katika mzunguko wa nyimbo za Bongo Fleva katika radio,mtaani,club na katika miito ya simu yaani ringtones.


Professor Jay atakuwa msanii wa kwanza kushoot video yake kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa ambavyo kampuni ya Visual Lab(Next Level) inayoongozwa na Adam Juma,imevipata hivi karibuni.
 
Alipokuwa aki'shoot video yake watu kibao walijitokeza ilikujihusisha na shughuli hiyo. Zidi kusikiliza KETAU EXPRESS kwenye radio taifa 92.9 (2pm-4pm) kwani  tutakupa wimbo huu mara hiyo hiyo..

No comments:

Post a Comment