![]() |
| DULLY SYKES |
Msanii chipukizi kutoka Ilala, mzee wa bongo fleva Dully Sykes amewashangaza wengi wakiwemo mashabiki wake wakuu wa Afrika mashariki. Baada tu ya kutangazwa kuwa mmoja wa watakaoshiriki kupigiwa kura
kwenye hatua ya awali ya mchujo wa tuzo za KILI TANZANIA MUSIC AWARDS.
Dully Sykes alidinda kushiriki huku akiwalamu wahusika kwa kitendo chao cha kumweka katika kinyang'anyiro
hicho wakati alishasema,
hataki kushiriki."Nilishawaambia sitaki kuwepo tena katika tuzo zao, tangu mwaka
juzi, lakini nashangaa kuona wanaendelea kuniweka tu, kwani wananiona
mimi ndio msanii pekee, wakati ule wa hits kama nyambizi, Hi na
zinginezo mbona hawakunipa tuzo? au walidhani mi ni msanii ambae
ningeishia kati tu, lakini baada ya kuona nipo na naendelea kuwepo ndio
wanajifanya kunitambua..nimesema sitaki.

Baadhi ya wasanii wanaowania tuzo la muziki wa Kilimanjaro mwaka 2011
wametangazwa huku wasanii Nasib Abdul maarufu kama ‘Diamond’ na Ali Kiba walitajwa
kuwania tuzo sita ikiwemo wimbo bora wa mwaka na mtumbuizaji bora wa kiume. Wadau wa muziki wataanza kupiga kura Februari 13 hadi Aprili 6.Tuzo hizi zikidhaminiwa na kilimanjaro beer kama kawa.....

No comments:
Post a Comment