Tuesday, 21 February 2012

JE KUNA BEEF KATI YA ALI K NA DIAMOND?

ALI KIBA
Tetesi zipo kutoka Bongo kwamba kuna beef kati ya wasnii wa muziki wa kizazi kipya kati ya Ali Kiba na Nassib Abdul aka Diamond.Chanzo cha beef ni kushtumiana kufuatia vocals katika nyimbo zao.

DIAMOND
Habari tulizonazo kwa sasa zinasema kwamba Ali Kiba anadai Diamond ndiye aliyeanza utata baada ya kufuta sauti yake kwenye rekodi ya Lala Salama ambayo alishiriki awali, ila baada ya hiyo ngoma kwenda redioni hakuskia sauti yake!

Kwa upande wa Diamond yeye anadai kuwa ngoma ya Kiba inayofanya vizuri hivi sasa Single Boy walifanya wote ila mwishowe hakuskia sauti yake na badala yake akaskia sauti ya Lady Jay Dee!

Diamond  sasa amezindua video mpya ya wimbo Mawazo ambayo imegharamia zaidi ya milioni tatu kutengenezwa na kampuni ya Visual Lab: Next Level chini ya usimamizi wa Adam Juma.

No comments:

Post a Comment