Friday, 10 February 2012

50 CENT NCHINI KENYA

Msanii wa mitindo ya rap anayekubalika duniani 50 Cent ambaye majina yake kamili ni Curtis James Jackson hapo jana alizuru mtaa wa mabanda wa Kibera katika ziara yake iliyoingia siku ya pili hivi leo. Hakuja kwa shughuli za utumbuizaji kama wanavyotarajia mashabiki wake bali ni kwa ziara ya kutoa msaada kwa janga la njaa iliyo chini ya mwavuli wa World Food Program. 

Msanii huyo amevuma duniani kwa nyimbo zake kama vile, 21 Questions, Get Rich or Die Trying na Window Shopper miongoni mwa nyingine.  Msanii huyu yumo kwenye hoteli ya kifahari ya Sankara hapa Nairobi.

No comments:

Post a Comment