Monday, 6 February 2012

Chipukizi Wajitokeza

Kundi la East Africa Upcoming Artists Association (EAUAA) chini ya uongozi wa Fernandos Kredgie limetoa wimbo mpya unaojulikana kama "Bado." ambao ni collabo iliyowashirikisha wasanii chipukizi sita wa humu nchini. 

Wimbo huu unazungumzia maswala ya amani, ufisadi na ustaarabu katika upigaji kura hasa ikizingatiwa ni mwaka wa uchaguzi. Akizungumza na meza ya Ketau express, kiongozi wa kundi hili Fernandos Kredgie, alisema kwamba "Wimbo huu umeimbwa kusistiza amani mwaka huu wa uchaguzi na kuwapatia changamoto vijana kutotumiwa na viongozi vibaya." 

Wasanii wengine walioshiriki katika wimbo huu ni K-Jeezy, G-Park, E-Vanso,CI na Kate ambapo katika wimbo wenyewe verse ya kwanza hadi ya mwisho ni mtawalio wa wasanii walivyo jipanga huku Fernandos Kredgie na Kate wakiwa wamefanya chorus.

Beat ya wimbo huu imefanywa na producer Godrick wa Springs Records Kitale, ilhali imerekodiwa na producer K-Mo wa Kamata Entertainment Nairobi. 

kundi hili lina jukumu la kukuza vipaji vya wasanii chipukizi ilikuakikisha wanafanya muziki unaodhamana kwa jamii.

kama wewe ni msanii chipukizi na ungependa kukuza talanta yako ya uimbaji, wasiliana na East Africa Upcoming Artists Association (EAUAA) kwenye Facebook, 0726627562,0705492838  au  fokredgie@gmail.com


1 comment: