Mwanadada aliyeibuka kwenye
shindano la Bongo Star Search, Baby Madaha, amejiunga rasmi kwenye Kundi
la TMK Wanaume Halisi Kujiunga TMK kumethibitishwa na mwanadada huyo pamoja na kiongozi Juma Kassim Ally Kiroboro aka
‘Sir Nature’.
Mwanadada huyo ambaye atakuwa wa kike pekee kwa kundi hilo alipoulizwa alikiri kufanya kazi na TMK Wanaume Halisi na
kuongeza kwamba mwaka huu ameamua kujipanga vyema zaidi.
Kwa upande wa Nature, alijibu: “Unauliza maembe kibada? Baby Madaha
ndiye first lady wa Halisi. Tumemchukua kwa sababu anaweza kazi.” Baby alifanya kazi mbalimbali ndani na nje ya
nchi lakini alipotoa ngoma yake inayokwenda kwa jina la Amore,
ilimtambulisha vema.
No comments:
Post a Comment